saudi arabia - Ukurasa 2

IQNA

IQNA – Ufalme wa Saudi Arabia umeanzisha mpango wake wa kila mwaka wa Mwezi wa Ramadhani katika ngazi ya kimataifa, unaojumuisha ugawaji wa nakala milioni 2.2 za Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3481945   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/16

IQNA – Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia amemteua kiongozi mmoja kutoka jamii ya Waislamu wa madhehebu ya Shia kuwa Waziri wa Uwekezaji wa nchi hiyo.
Habari ID: 3481937   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/15

IQNA – Wakati mamilioni ya Waislamu duniani kote wakisubiri kwa hamu kuwasili kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani na maandalizi yakiendelea, hesabu za kiastronomia zinaonesha kuwa mwisho wa mwezi wa Shaaban 1447 Hijria kiastronomia utasadifiana na Jumatano, Februari 18.
Habari ID: 3481914   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/10

IQNA – Idadi ya wageni wa wa kimataifa waliotekeleza ibada ya Hija ndogo ya Umrah katika Ufalme wa Saudi Arabia ilifikia milioni 19.5 mwaka 2025, kwa mujibu wa takwimu rasmi, huku kiwango cha kuridhika na huduma kikizidi asilimia 90.
Habari ID: 3481882   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/02

Rais wa Iran katika mazungumzo na Bin Salman wa Saudia
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian amesema kuwa katika ghasia za hivi karibuni, maadui, yaani Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, walilenga kuigeuza Iran kuwa Syria au Libya nyingine,"
Habari ID: 3481858   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/28

IQNA-Msikiti wa Imam Mahdi (AS) uliopo Sihat, katika Mkoa wa Mashariki wa Saudi Arabia, ulijengwa takribani miaka 132 iliyopita, na hivyo kuwa miongoni mwa nyumba kongwe za ibada katika eneo hilo.
Habari ID: 3481806   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/15

IQNA – Wageni wa Maonyesho ya 48 ya Vitabu Kimataifa mjini Kuwait wamepewa zawadi ya nakala zaidi ya 5,000 za Qur'ani Tukufu. Banda la Wizara ya Mambo ya Kiislamu ya Saudi Arabia limesambaza nakala hizo, kwa mujibu wa taarifa ya Al-Madinah.
Habari ID: 3481590   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/30

IQNA – Sala ya Istisqa (swala ya kuomba mvua) imeswaliwa leo Alhamisi, kufuatia sunnah ya Mtume Muhammad (SAW) ya kuomba rehema ya Mwenyezi Mungu kupitia ibada ya pamoja. Swala hiyo imeswaliwa kufuatia ombi la Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia
Habari ID: 3481508   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/13

IQNA – Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi Arabia siku ya Jumapili imezindua rasmi Mkutano na Maonesho ya 5 ya Hajj kwa mwaka 1447 Hijria, yanayoendelea kuanzia tarehe 9 hadi 12 Novemba 2025 katika jiji la Jeddah, chini ya kauli mbiu “Kutoka Makkah Hadi Ulimwenguni.”
Habari ID: 3481495   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/10

IQNA – Nyumba ya Makumbusho ya Sanaa za Kiislamu mjini Jeddah, maarufu kwa jina la Dar al-Funun al-Islamiyyah, imeandaa maonesho ya hati adimu za Qur’ani Tukufu pamoja na kazi za sanaa zinazodhihirisha uhusiano wa kihistoria kati ya imani ya Kiislamu, uzuri wa sanaa, na ustadi wa mikono.
Habari ID: 3481479   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/07

IQNA – Mwanazuoni mwenye msimamo wa kihafidhina na aliye katika miaka ya tisini ameteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa kidini au Mufti Mkuu nchini Saudi Arabia, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.
Habari ID: 3481406   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/23

IQNA-Katika mwezi wa Rabi al-Awwal 1447 Hijria, Misikiti Miwili Mitakatifu—Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume (SAW) huko Madina, imepokea jumla ya waumini 53,572,983, wakiwemo waumini na mahujaji, kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Huduma za Misikiti Miwili Mitakatifu.
Habari ID: 3481291   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/27

IQNA – Idadi ya safari za ndege zinazowasafirisha waumini wa ibada ya Umrah kutoka Iran kwenda Saudi Arabia imeongezeka tangu mwanzo wa wiki hii.
Habari ID: 3481287   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/26

IQNA – Hatua ya mwisho ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu imeanza Alhamisi katika mji mkuu wa Afrika Kusini, ikiwakutanisha washiriki kutoka nchi 29.
Habari ID: 3481250   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/19

IQNA – Baraza la Mipango na Uratibu kutoka ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu katika Masuala ya Hija na Ziara, pamoja na Shirika la Hija na Ziara la Iran, wameanza maandalizi ya safari ya Hija ya mwaka ujao.
Habari ID: 3481177   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/03

IQNA – Maonyesho ya Kimataifa na Makumbusho ya Maisha ya Mtume Muhammad (SAW) pamoja na Ustaarabu wa Kiislamu yamezinduliwa katika Mnara wa Saa, katika mji mtukufu wa Makkah, siku ya Jumanne.
Habari ID: 3481152   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/29

IQNA – Washiriki wa Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Mfalme Abdulaziz wametembelea misikiti ya kihistoria na maeneo ya turathi katika mji wa Madina, kama sehemu ya programu ya kitamaduni iliyoandaliwa na mamlaka za Saudi Arabia.
Habari ID: 3481108   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/19

IQNA – Toleo la 45 la mashindano ya kimataifa ya Qur’ani linaloendelea mjini Makkah limeendelea Jumatatu katika Msikiti Mtukufu (Masjid al Haram), likishuhudia washiriki 18 wakionesha vipaji vyao vya Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3481074   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/12

IQNA – Roboti za kielektroniki zinazoweza kuingiliana na watumiaji zimetumika katika toleo la 45 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yanayofanyika Makkah kwa lengo la kuboresha huduma kwa wageni.
Habari ID: 3481072   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/11

IQNA – Jukwaa la kielimu la Qur’ani kwa ajili ya wasiozungumza Kiarabu linazinduliwa nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3481069   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/11