IQNA

Papa amtunuku Balozi wa Iran Vatican nshani ya juu ya kidiplomasia

21:11 - May 13, 2026
Habari ID: 3482235
IQNA – Papa Leo XIV amemtunuku Hujjatul‑Islam Mohammad Hossein Mokhtari, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Vatican, nishani ya juu zaidi ya kidiplomasia ya Vatican.

Nishani hiyo inayojulikana kama Papal Order of the Piano ni tuzo ya heshima ya Vatican iliyoanzishwa mwaka 1847 na Papa Pius IX.

Tuzo hiyo inahesabiwa miongoni mwa nishani za juu kabisa katika mfumo wa heshima wa Vatican, na kwa kawaida hutolewa kwa mabalozi na watu mashuhuri waliotoa mchango katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia pamoja na kuendeleza amani na mazungumzo ya kimataifa.

Kwa mujibu wa ubalozi wa Iran, kutunukiwa kwa nishani hiyo kumefanyika katika kipindi ambacho msimamo wa hivi karibuni wa Papa Leo XIV wa kubainisha ukweli na kulaani mashambulizi ya Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran unaonekana kwenda sambamba na juhudi za Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Vatican katika kufafanua ujumbe wa amani, uadilifu na kupinga uchochezi wa vita.

3497443

Habari zinazohusiana
captcha