IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Qur’ani ya Makka kutangazwa Jumatano

23:14 - August 20, 2024
Habari ID: 3479307
IQNA - Sherehe za kufunga Mashindano ya Kimataifa ya 44 ya Mfalme Abdulaziz ya Kuhifadhi, Kusoma na Kutafsiri Qur'ani zitafanyika katika Msikiti Mkuu wa Makka siku ya Jumatano.

Naibu gavana wa Makka atawatunuku washindi wa hafla hiyo ya kimataifa ya Qur'ani.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu ya Saudia Abdullatif bin Abdulaziz Al-Sheikh, ambaye ndiye msimamizi wa mashindano hayo, alisema washiriki 174 kutoka nchi 123 walishiriki katika mashindano ya mwaka huu, idadi kubwa zaidi kushiriki katika historia ya mashindano hayo.

Waziri huyo alisema mashindano hayo yanaashiria namna Saudia inavyowaenzi wanaohifadhi Qur’ani Tukufu. Jumla ya zawadi kwa washiriki wote katika mashindano hayo ni takribani dola milioni moja.

Mohammad Mehdi Rezaei na Mohammad Hossein Behzadfar wanawakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hafla ya kimataifa ya Qur'ani.

3489572

Habari zinazohusiana
captcha