IQNA

Shughuli za Qur'ani Tukufu

Wanafunzi wa Kiafrika washiriki kozi ya Qur'ani huko Najaf, Iraq

14:03 - November 03, 2022
Habari ID: 3476030
TEHRAN (IQNA) – Kozi ya kiwango cha juu ya Qur’ani Tukufu imeandaliwa kwa ajili ya wanafunzi wa Afrika wanaosoma sayansi ya Kiislamu katika vyuo vya Kiislamu vya mji mtakatifu wa Najaf, Iraq.

Idara ya Kitamaduni na Kielimu ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas (AS) imeandaa kozi hiyo chini ya usimamizi wa Kituo cha Masomo ya Afrika.

Sayed Sattar Al-Shamari, mkurugenzi wa kituo hicho, alisema idadi ya wasomi kutoka vyuo vikuu tofauti vya Iraqi wanafundisha masomo ya kozi hiyo.

Alisema kozi hiyo ni moja ya mfululizo wa programu za Qur'ani zinazofanyika kwa wanafunzi wa Kiafrika wanaosoma sayansi za Kiislamu mjini humo, tovuti ya Al-Kafeel iliripoti.

Al-Shamari ameongeza kuwa programu hizo zinalenga kukuza na kufafanua mafundisho ya Quran kwa wanafunzi wa seminari kutoka nchi za Afrika.

Kozi hiyo inasaidia kuongeza maarifa ya wanafunzi wa Kurani na pia itawanufaisha katika masomo yao ya seminari, alibaini.

Wanafunzi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wanasoma masomo ya sayansi ya Kiislamu katika Hauza  ya Kiislamu (Seminari) ya Najaf, mojawapo ya seminari maarufu za Madhehebu ya Kiislamu ya Shia duniani.

Baada ya kumaliza masomo yao, wengi wao hurejea nchini mwao kueneza mafundisho sahihi ya Uislamu.

.

 African Seminary Students Take Advanced Quranic Course in Najaf

 African Seminary Students Take Advanced Quranic Course in Najaf

 African Seminary Students Take Advanced Quranic Course in Najaf

 African Seminary Students Take Advanced Quranic Course in Najaf

 

4096335

Kishikizo: najaf iraq qurani tukufu
captcha