IQNA

Pigia Kura Kauli Mbiu ya Maonyesho ya 33 ya Kimataifa ya Qur’an Tukufu ya Tehran

15:58 - January 07, 2026
Habari ID: 3481780
IQNA – Kamati ya maandalizi ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’an Tukufu mjini Tehran imetoa mwito kwa umma kushiriki katika kuchagua kauli mbiu ya toleo la 33 la tukio hili kubwa la Qur’an.

Lengo ni kuvutia ushiriki wa jumuiya ya Qur’an, hususan wanazuoni na wasanii, ili maonyesho haya ya kimataifa yawe na hadhi na uzuri zaidi.

Kwa mujibu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Habari ya Kituo Kikuu cha Qur’an na Etrat cha Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran, washiriki wanaweza kupiga kura kuchagua kauli mbiu kutoka miongoni mwa chaguo nane zifuatazo:

  1. Aya zinakuita

  2. Kufahamu aya, kufanikisha vilele

  3. Qur’an na Etrat; mhimili wa umoja

  4. Pamoja na Qur’an hadi mbinguni

  5. Qur’an, Kitabu cha mwamko

  6. Qur’an chanzo cha maisha na matumaini

  7. Sisi na Qur’an

  8. Kutoka Aya hadi Kioo

Muda wa kushiriki utaisha tarehe 10 Januari 2026, na wanaotaka kushiriki wanaweza kujiandikisha kupitia tovuti www.iqfa.ir.

Baada ya kura kukamilika, kauli mbiu bora itatangazwa rasmi kama kauli mbiu ya Maonyesho 33 ya Kimataifa ya Qur’an Tukufu, na washiriki 10 watazawadiwa tuzo muhimu kupitia droo.

Maonyesho haya hufanyika kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani chini ya Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ya Iran. Yakiambatana na vipindi maalumu, warsha za kielimu, makongamano ya Qur’an, na shughuli mahsusi kwa watoto na vijana, maonyesho haya yanalenga kueneza dhana na shughuli za Qur’an.

Aidha, jukwaa hili hutumika kuonyesha mafanikio ya hivi karibuni ya Qur’an nchini Iran pamoja na bidhaa mbalimbali zinazohusiana na kuendeleza Kitabu Kitukufu.

3495985

Habari zinazohusiana
captcha