
Akizungumza na IQNA, Ali Reza Tavallayi alisema kuwa miongoni mwa majukumu ya taasisi hiyo ni kubuni safari zenye malengo mahsusi kwa “Balozi wa Qur'ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran”, pamoja na kuanzisha Chuo cha Kimataifa cha Qur'ani Tukufu.
Amesema kuwa taasisi hiyo imechochewa na maelekezo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, anayesisitiza ulazima wa kuweka Qur'ani katika kitovu cha harakati ili kuutekeleza ujumbe wa undugu wa Kiislamu katika ngazi za kikanda na kimataifa.
“Taasisi hii imeundwa kwa msukumo wa mkazo wa Kiongozi Muadhamu juu ya nafasi ya kati ya Qurani, Al‑Kaaba na Mtume Muhammad (SAW) katika kuleta mshikamano kati ya madhehebu mbalimbali ya Kiislamu, na tunajitahidi kuuhamisha mtazamo huu kutoka nadharia kwenda katika utekelezaji wa vitendo,” alisema Tavallayi.
Aliongeza kuwa Taasisi ya Diplomasia ya Qur'ani ni chombo huru kisichotegemea bajeti ya serikali, lakini kinaungwa mkono kiroho na kushirikiana na taasisi kama Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu, pamoja na taasisi nyingine za kitamaduni, ikiwemo Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu.
Tavallayi alibainisha kuwa baada ya kutolewa kwa amri ya uteuzi wa Balozi wa Qur'ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa bingwa wa Qur'ani Hamed Shakernejad, ilionekana kwa dhahiri haja ya kuwepo muundo thabiti wa kutoa maudhui rasmi shughuli zake na ndipo taasisi hiyo ilipoanza rasmi shughuli zake ndani ya muktadha huo.
Akisisitiza kuwa mtazamo wao hauishii katika kuandaa matukio ya ishara tu, alisema:
“Tunajitahidi kuutekeleza kwa vitendo dhana ya undugu wa Kiislamu. Kwa msingi huo, kila safari ya Balozi wa Qur'ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kwa muundo makini wa maudhui. Kabla ya safari, hali ya kitamaduni, kidini na kijamii ya nchi lengwa huchunguzwa; mtazamo wa watu wa nchi hiyo kuhusu Iran huchambuliwa; na ujumbe unaopaswa kufikishwa na jamii ya Qur'ani ya Iran huandaliwa kwa utaalamu.”
Habari inayohusiana:
Aliendelea kusema kuwa maudhui hayo huwasilishwa kwa Balozi wa Qur'ani ili ayatumie kwa ubunifu na busara binafsi katika mikutano na vikao vya Qur'ani.
“Lengo ni kuhakikisha kuwa uwepo wa mwakilishi wa jamii ya Qur'ani ya Iran katika nchi nyingine hauwi safari ya usomaji wa Qur'ani pekee, bali unakuwa mjumbe wa ujumbe wa umoja, huruma na mazungumzo ya kitamaduni,” aliongeza.
Tavallayi pia alisisitiza kuwa taasisi hiyo inaamini diplomasia ya Qur'ani inapaswa kuwa hai pia katika nyakati za migogoro ya kijamii na kibinadamu, na itumie lugha ya huruma na mshikamano kuimarisha mafungamano kati ya mataifa ya Kiislamu.
4336304