IQNA

Hamed Shakernejad ateuliwa kuwa Balozi wa Kimataifa wa Qur’ani wa Iran

17:23 - March 07, 2025
Habari ID: 3480323
IQNA – Qari na hafidh maarufu wa Qur’ani Tukufu kutoka Iran, Ustadh Hamed Shakernejad, ametajwa kuwa balozi wa kimataifa wa Qur’an wa Iran.

Uteuzi huo ulitangazwa na Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), Hujjatul-Islam Mohammad Mehdi Imanipour, wakati wa Mkutano wa Tatu wa Qur’ani huko Tehran, ulioitwa "Mkutano wa Qur’ani wa Ulimwengu wa Kiislamu: Mbinu ya Kimkakati kwa Kuleta Umma Uliounganika."

Hati rasmi ilisema, "Kwa kuzingatia uwezo wako wa kipekee, uzoefu wenye thamani, na shughuli nzuri za Qur’ani katika uwanja wa usomaji na kueneza mafundisho yenye nuru ya Qur’ani Tukufu, hasa katika ngazi ya kimataifa, umechaguliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Katika Masuala ya Qur’ani Tukufu."

Barua hiyo ilielezea jukumu kuu la Shakernejad, ambalo ni "kuendeleza diplomasia ya Qur’ani kwa kutambulisha na kukuza utamaduni wa Qur’ani Tukufu kama mhimili unaounganisha Umma wa Kiislamu."

"Tunamuomba Mwenyezi Mungu akupa mafanikio katika kutekeleza jukumu hili la kitamaduni na kiroho," aliongeza Imanipour.

Shakernejad ana shahada ya Uzamivu au PhD katika Mafunzo ya Qur’ani na ni msomaji wa Qur’ani mbali na kuwa Hafidh. Amewahu kushika nafasi za juu katika mashindano mengi ya kimataifa ya Qur’ani.

Mkutano wa Tatu wa Qur’ani huko Tehran ulifanyika Machi 6, ukiwa na zaidi ya wanaharakati wa Qur’ain hamsini kutoka nchi 24, uliandaliwa na Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu.

Mkutano huo ulikuwa sehemu ya sehemu ya kimataifa ya Maonyesho ya 32 ya Kimataifa ya Qur’an Tukufu huko Tehran.

Washiriki walijumuisha wasomi wa Quran kutoka Iran, Afghanistan, Algeria, Umoja wa Falme za Kiarabu, Indonesia, Uganda, Italia, Bosnia na Herzegovina, Pakistan, Tajikistan, Thailand, Uturuki, Chad, Uchina, Urusi, Côte d'Ivoire, Iraq, Qatar, Cambodia, Guinea, Lebanon, Nigeria, na India.

./3492203

Habari zinazohusiana
captcha