
Wizara hiyo imetangaza majina ya washindi wa mashindano maalumu kwa wanaojifunza Qur’ani katika vituo vya kuhifadhi Qur’ani, kwa mujibu wa ripoti ya El-Balad.
Haya yalikuwa ni mashindano ya nne makubwa ya Qur’ani yaliyoandaliwa miongoni mwa wanafunzi wa vituo vya kuhifadhi Qur’ani, katika makao makuu ya Chuo cha Kimataifa cha Awqaf nchini humo.
Mashindano hayo yalifanyika kuanzia tarehe 21 hadi 23 Aprili 2026, huku hatua ya fainali ikishuhudia ushindani wa hali ya juu miongoni mwa washiriki katika nyanja za hifdh (uhifadhi wa Qur’ani), qiraa (usomaji sahihi), na tajwid.
Wizara ya Awqaf ilieleza kuwa mwishoni mwa mashindano hayo, washiriki waliobainika kuwa na umahiri mkubwa katika kuhifadhi pamoja na utendaji mzuri walifanikiwa kushinda, jambo linalodhihirisha nafasi ya msingi ya vituo vya kuhifadhi Qur’ani ndani ya jamii.
Aidha, wizara imesisitiza kuwa vituo hivyo vina mchango madhubuti katika kuandaa wahudumu wa Qur’ani waliobobea kielimu na kida‘wah, wenye uwezo wa kueneza mwangaza na uongofu wa Qur’ani katika jamii, pamoja na kulea shakhsia za kizalendo.
Mashindano hayo ni sehemu ya mpango wa wizara wa kuwaunga mkono wahudumu wa Qur’ani, kueneza mafundisho ya dini kwa usahihi, na kuwahimiza vijana na baleghe kuelekea kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kukifahamu, na kutafakari mafunzo yake.
Wizara imefafanua kuwa tuzo zilizotolewa kwa washindi ni namna ya kuwathamini na kuwapa motisha ya kuendelea kufanya vyema katika kuitumikia Qur’ani Tukufu na kushikamana na maadili ya juu ya dini.
Vilevile, wizara imetangaza tena uungaji mkono wake kamili kwa vituo vya kuhifadhi Qur’ani na kwa kuendeleza programu zake za kielimu na kimafunzo, kwa lengo la kulea kizazi cha wahudumu wa Qur’ani katika jamii nzima ya Misri.
3497403