IQNA

Mamilioni ya Wairani washiriki Tasu'a ya Imam Hussein (AS)

14:07 - June 24, 2026
Habari ID: 3482397
IQNA-Wairani katika mji mkuu Tehran, majiji, miji na vijiji vyote nchini usiku wa kuamkia leo walikusanyika misikitini na katika vituo vya kidini na barabarani katika marasimu ya kuadhimisha Tasu'a, siku ya tisa ya mwezi Muharram, kuelekea kwenye Siku ya Ashura ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW).

Waombolezaji katika kona zote za Iran wametangaza kushikamana kwao na Ahlul Bait wa Mtume wetu Muhammad (SAW), mafundisho sahihi ya Uislamu na kutetea malengo ya Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib ya kupinga dhulma na kupambana na uonevu na upotoshaji.

Waombolezaji nchini Iran wakiwa wamevaa nguo nyeusi, kama ishara ya huzuni na majonzi, walikuwa wakibubujikwa na machozi kwa kukumbuka dhulma iliyofanywa na madhalimu dhidi ya Imam Hussein (AS), watu wa nyumba yake na wafuasi wake watiifu. Aidha mwaka huu maadhimisho hayo yana muelekeo wa kipekee baada ya vita vya siku 40 vya kichokozi Marekani na Israel dhidi ya Iran ambavyo vilianza tarehe 10 Ramadhani saw ana Februari 28.

Wananchi walioshiriki katika hafla za maombolezo mwaka huu wameapa kufungamana na malengo matukufu ya Kiongozi Muadhamu aliyeuawa shahidi vitani Imam Khamenei (MA). Aidha wametangaza kumtii kikamilifu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeteuliwa Ayatullah Mujtaba Khamenei

Nara kuu katika maombolezo ya sasa ya Muharram ni kulaani mashambulizi na ukatili wa Marekani na Israel dhidi ya umma na mataifa ya Kiislamu, hususan Iran, Palestina na Lebanon na kula tena kiapo cha utiifu kwa ajili ya kudumisha mapambano ya mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW).

Kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu wa Muharram mamlaka za Iraq zimekuwa zikijitayarisha kwa ajili ya kupokea mamilioni ya mazuwari na Waislamu wanaoendelea kumiminika katika mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya Siku za Tasu'a na Ashura na kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (AS).

Marasimu ya Muharram hushika kasi zaidi tarehe 9 na 10 Mfunguo nne ambapo mamilioni ya Waislamu kutoka maeneo mbalimbali ya dunia huwasili katika mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya maombolezo na kukumbuka tukio chungu la kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na watu wengine wa familia ya Mtume. 

Kilele cha maombolezo ya Muharram kitakuwa tarehe 10 siku inayojulikana kwa jila la Ashura ambapo Imam Hussein (AS) na watu wengine wa familia ya Mtume Muhammad na wafuasi wao waaminifu waliuawa kikatili baada ya mapambano ya kishujaa yaliyobakia hai katika historia ya wanadamu.

Imam Hussein (AS), akiwa pamoja na watu wengine wa familia ya Mtume Muhammad (SAW) na masahaba zake waaminifu waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram katika mapambano ya siku ya Ashura dhidi ya utawala dhalimu wa Yazid bin Muawiya.

3497959

captcha