Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa X, Albanese aliandika: “Hati ya haraka ya kukamatwa inapaswa kutolewa dhidi ya mhalifu huyu wa kivita aliyekiri jinai zake mwenyewe.” Alisisitiza kuwa hali ya kutoguswa na sheria (impunity) wanayofurahia viongozi wa utawala wa Kizayuni inazidisha kiwango cha uharibifu unaofanywa dhidi ya mfumo wa kimataifa ulioundwa kulinda haki za binadamu kwa wote.
Wito huo umekuja kufuatia matamshi ya Katz kupitia vyombo vya habari, ambapo akizungumzia hali ya Lebanon, alisema: “Nilisema kuwa kusini mwa Lebanon itakuwa kama Gaza, na tutatumia mtindo wa Rafah; tutaharibu kila kitu huko, na ndivyo tulivyofanya kwa hakika.”
Katz aliongeza kuwa miundombinu iliharibiwa na nyumba katika vijiji 24 kando ya mpaka, baadhi zikiwa na historia ya mamia ya miaka, zilifutika kabisa. Alibainisha kuwa jeshi la Kizayuni liliharibu vijiji hivyo kwa utaratibu maalum kwa kutumia tingatinga na vilipuzi, na kwamba asilimia 90 ya makazi yote yamepotea, huku nyumba kati ya 15,000 na 20,000 zikiharibiwa vibaya.
3498232