
Hafla hiyo, iliyoandaliwa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Wapalestina, ilifanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ili kusisitiza athari za kudumu za Nakba, uhamishaji mkubwa na kunyang’anywa kwa Wapalestina wakati wa kuanzishwa kwa utawala haramu wa Israel mwaka 1948.
Akilihutubia mkutano huo, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bi. Annalena Baerbock, alielezea Nakba kama “maumivu” ya kihistoria ya kudumu yanayoendelea kwa vizazi.
“Waliondolewa majumbani mwao, nyumba zao zikafanywa kifusi, maisha yao na riziki yao vikavurugwa. Katika muda mfupi, taifa zima likatawanywa,” alisema.
“Ni maumivu yanayoendelea kwa vizazi na maelfu ya kilomita. Ni maumivu ambayo haki yenye maana tu ndiyo inaweza kuleta afueni.”
Bi. Baerbock alisema kuwa suala hilo bado lina umuhimu mkubwa kwa sababu mateso ya Wapalestina hayajaisha.
Pia alisisitiza wajibu unaoendelea wa Umoja wa Mataifa kutafuta suluhisho la haki kwa kadhia ya Palestina.
“Mojawapo ya majukumu ya kwanza ya Umoja wa Mataifa ilikuwa ni kutafuta suluhisho la haki kwa mizozo na majanga duniani kote, ikiwa ni pamoja na swala la Palestina,” Bi. Baerbock alisema. “Kwa miaka 78 mirefu, taasisi hii, pamoja na michakato mingine mingi ya amani, imefanya kazi kushughulikia kadhia ya Palestina na utawala wa Israel.”
Aliwataka wanachama wasipoteze mwelekeo juu ya janga la kibinadamu huko Gaza, ambalo alielezea kuwa “janga la kutisha” licha ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano Oktoba iliyopita.
“Usitishaji mapigano, ambao haumaanishi amani, bali mauaji zaidi, hata ya watoto, si amani na si usitishaji mapigano,” alisema. “Ni mwendelezo wa moto.”
Bw. Khaled Khiari, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mashariki ya Kati, Ulaya, Amerika, Asia na Pasifiki, pia alionya kuwa hali huko Gaza bado ni mbaya. “Hali huko Gaza leo ni janga la ukubwa mkubwa,” Bw. Khiari aliwaambia washiriki.
Aliongeza kuwa usitishaji mapigano unabaki kuwa dhaifu na raia wanaendelea kuteseka.
3497475