IQNA

Tarjuma za Qur'ani kutoka Malaysia zapelekzwa Marekani, Afrika Magharibi

9:51 - February 07, 2026
Habari ID: 3481898
IQNA-Malaysia inaendelea kutumia diplomasia ya kitamaduni na kidini kwa kusambaza nakala 40,000 za Qur’ani Tukufu zenye tarjuma katika lugha mbali mbali huko Marekani na Afrika Magharibi.

Nchi hiyo ya Asia ya Kusini Mashariki siku ya Ijumaa ilisafirisha nakala 40,000 za Qur’ani zenye tafsiri kwenda Washington, Marekani, pamoja na Ivory Coast na Ghana, hatua inayoakisi dhamira endelevu ya Malaysia ya kueneza maadili ya Kiislamu na elimu ya Qur’ani katika ngazi ya kimataifa.

Waziri wa Masuala ya Kidini, Zulkifli Hassan, alisema usafirishaji huo ulifanyika kupitia Kituo cha Nasyrul Quran, kwa ushirikiano na Restu Foundation pamoja na wahisani wa waqf.

Alieleza kuwa mpango huo ni sehemu ya mradi wa Mshikamano wa Waqf wa Qur’ani Milioni Moja, uliohamasishwa na Waziri Mkuu Anwar Ibrahim, unaolenga kusambaza nakala za Qur’ani zenye tafsiri katika lugha mbalimbali duniani kote.

“Usafirishaji huu wa nakala hizi za Qur’ani bali ni jukumu la da‘wah na ubinadamu,” alisema. “Unawakilisha nafasi ya Malaysia kama mshirika wa kimkakati katika kuimarisha uelewa wa Uislamu kama dini ya rehema kwa walimwengu wote.”

Alisema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa usafirishaji wa makontena mawili ya nakala za Qur’ani kwenda nchi hizo tatu, iliyofanyika Putrajaya siku ya Ijumaa.

Zulkifli aliongeza kuwa hadi sasa, Malaysia imesambaza tarjuma za Qur’ani katika lugha mbalimbali kwa zaidi ya nchi 40.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Mtendaji wa Restu Foundation, Abdul Latiff Mirasa, alisema usafirishaji huo unaakisi dhamira endelevu ya taasisi hiyo katika kuunga mkono azma ya Malaysia ya kuwa kitovu cha kimataifa cha uchapishaji, tafsiri na usambazaji wa Qur’ani.

Habari inayohusiana:

“Usafirishaji huu umefikisha jumla ya Misahafu iliyosambazwa kupitia taasisi na mashirika mbalimbali kufikia 553,966,” alisema.

Shehena hiyo ilijumuisha nakala 20,000 za Qur’ani zenye tarjuma za Kiingereza, Kihispania, Kihispania cha Ulaya na Kihispania cha Amerika ya Kusini kwa ajili ya Marekani (Washington), pamoja na nakala 20,000 zenye tafsiri za Kifaransa na Kiingereza kwa ajili ya kusambazwa katika Ivory Coast na Ghana.

3496321

Habari zinazohusiana
captcha