Ijumaa usiku Uturuki ilikuwa medani ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli kuiangusha serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Reccep Tayyib Erdogan.
Habari ID: 3470457 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/17
Gingrich, Spika wa Zamani wa Bunge la Marekani
Spika wa zamani wa Kongresi ya Marekani amesema kuwa Waislamu wanaoshikamana na sheria za Kiislamu wanapaswa kufukuzwa nchini Marekani.
Habari ID: 3470456 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/16
Watu wasiopungua 84 wameripotiwa kuuawa katika hujuma ya kigaidi katika mji wa Nice kaskazini mwa Ufaransa.
Habari ID: 3470455 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/15
Waislamu nchini Uingereza wamebainisha hofu ya kuhusu kuteuliwa Bi.Theresa May kama Waziri Mkuu kutokana na sera zake haribifu kwa jamii ya Waislamu nchini humo.
Habari ID: 3470454 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/14
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeitaja kuwa bandia habari iliyoenezwa kuwa limeitaja dini tukufu ya Kiislamu kuwa ndiyo dini ya amani zaidi duniani.
Habari ID: 3470453 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/13
Wabunge Uingereza
Wabunge nchini Uingereza wameutaka utawala wa Saudia na nchi nyingine za Kiarabu zizuie matajiri wa nchi hizo kulifadhili kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
Habari ID: 3470452 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/13
Saudi Arabia imemkamata mwanazuoni mkubwa wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.
Habari ID: 3470451 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/13
Sheikh Mohammad Hashim Al Hakim, mwanachama wa Jumuiya ya Maulamaa wa Sudan ametahadharisha kuhusu kusambazwa nakala za Qur'ani nchini humo ambazo zina makosa ya chapa.
Habari ID: 3470450 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/12
Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu Uingereza ametoa taarifa na kusema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh halina uhusiano wowote na Uislamu.
Habari ID: 3470448 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/12
Katibu wa Baraza la Ustawi wa Utamaduni wa Qur’ani Iran amesema Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu ni tukio la kipekee katika Ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3470445 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/10
Kadinali Malcolm Ranjith wa Kanisa Katoliki Sri Lanka amempongeza hayati Imam Khomeini MA kwa kusimama kidete kukabiliana na ubabe wa Marekani sambamba na kudumisha heshima na uhuru wa Iran.
Habari ID: 3470444 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/10
Nakala 480,000 za Qur’ani Tukufu zimechapishwa nchini Iran katika miezi mitatu ya kwanza ya Kalenda ya Kiirani kuanzia Machi 21 hadi Juni 20.
Habari ID: 3470443 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/10
Magaidi wa ISIS Alhamisi walishambulia ziara la mjukuu wa Mtume Muhammad SAW katika mji wa Balad ulioko umbali wa kilomita 80 kutoka Baghdad na kuua watu wasiopungua 40.
Habari ID: 3470441 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/08
Huku Waislamu duniani wakisherehekehea siku kuu ya Idul Fitr, msomi wa Kiislamu Kenya ameitunukia jamii ya Waluo Qur'ani Tukufu iliyotafsiriwa (tarjumiwa) kwa lugha ya Kiluo.
Habari ID: 3470440 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/08
Bunge la Umoja wa Ulaya limelaani vikali kuendele akukandamiwa Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar.
Habari ID: 3470438 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/08
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiisalmu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema chanzo kikuu cha vita, ukosefu wa usalama katika eneo la Kusini mwa Asia na Ulimwengu wa Kiislamu ni madola makubwa ya kiistikbari yakiongozwa na Marekani.
Habari ID: 3470437 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/06
Maafisa wa ngazi za juu katika ufalme wa Saudi Arabia wamekuwa wakiingiza dawa za kulevya nchini humo kwa kutumia mabasi yanayowabeba mahujaji, imefichuliwa.
Habari ID: 3470436 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/06
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema leo kuwa taifa la Iran litaendelea kusimama kidete dhidi ya maadui wote kwa ajili ya kutetea taifa linalodhulumiwa la Palestina.
Habari ID: 3470435 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/06
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani hujuma za kigaidi zilizojiri Jumatatu Saudi Arabia likiwemo ikiwemo karibu na Msikiti wa Mtume SAW katika mji mtakatifu wa Madina.
Habari ID: 3470434 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/05
Leo ni Siku Kuu ya Idul Fitr; baada ya siku 30 za Mwezi wa Ramadhani wenye baraka tele na neema nyingi za Mwenyezi Mungu pamoja na baraka zake za kimaanawi. Huu ni mwanzo halisi wa kuelekea katika ubora wa mwanadamu. (Ayatullah Khamenei: 13/10/2007)
Habari ID: 3470433 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/05