Harakati za Qur'ani
IQNA - Sherehe ilifanyika mashariki mwa Kosovo kuwaenzi wasichana 44 ambao wamehitimu kutoka kozi za Qur'ani.
Habari ID: 3479672 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/30
Waislamu Afrika Kusini
IQNA - Msikiti wa Barabara Kuu ya Claremont (CMRM) nchini Afrika Kusini umeadhimisha mwaka wa 170 tokea ujengwe. Maadhimisho hayo yamejumuisha kwa mkusanyiko wa Khatm al-Quran (kusoma Qur'ani Tukufu tokea mwanzo hadi mwisho) na kuenziwa wale wote ambao wamechangia katika historia ya msikiti huo.
Habari ID: 3479671 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/30
IQNA-Muungano wa viongozi wa Waislamu wenye asili ya Afrika nchini Marekani wamewataka wapiga kura kumkataa Makamu wa Rais Kamala Harris katika azma yake ya kuwania urais wa Marekani 2024 kutokana na sera yake ya kuunga mkono mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza.
Habari ID: 3479633 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/22
Ubaguzi Marekani
IQNA - Kundi la kutetea haki za Waislamu Marekani limewasilisha malalamiko katika Idara ya Elimu ya Marekani, likitaka uchunguzi ufanyike iwapo Chuo Kikuu cha Michigan kimeshindwa kuwalinda wanafunzi wa Palestina, Waarabu, Waislamu na Waasia Kusini kutokana na kubaguliwa.
Habari ID: 3479574 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/11
IQNA – Kubomolewa Msikiti wa miaka 1,200 Dargah (makaburi matakatifu ya Waislamu), katika wilaya ya Gir Somnath, Gujarat ya India kumeibua maandamano makubwa.
Habari ID: 3479517 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/09/30
Umoja wa Kiislamu
IQNA - Rais wa Baraza la Ushauri la Mashirika ya Kiislamu ya Malaysia (MAPIM) alitoa wito kwa nchi za Kiislamu kutuma majeshi yao kukabiliana na ukatili wa utawala wa Israel huko Gaza.
Habari ID: 3479487 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/09/25
Wiki ya Umoja wa Kiislamu
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, adui analeta mgawanyiko na mifarakano kati yetu na kubainisha kwamba, Waisraeli milioni 2 au 3 wanawaangamiza Waislamu, wanaua wanawake na watoto, wazee na vijana na wagonjwa, wanapiga mabomu hospitali na misikiti na sisi tumekaa tu na kutazama, kwa sababu hatuna umoja na ndio maana Israel inathubutu kufanya jinai hizi.
Habari ID: 3479453 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/09/19
Uislamu na Jamii
IQNA - Magereza yote nchini Kenya yameagizwa kutenga ardhi kwa ajili ya ujenzi wa misikiti na makanisa.
Habari ID: 3479403 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/09/09
Watetezi wa Palestina
IQNA - Mamlaka za Ufaransa zilimkamata na kisha kumwachilia muuguzi Imane Maarifi, ambaye alitumia siku 15 kujitolea kama tabibu katika Ukanda wa Gaza wakati huu wa vita vya mauaji ya kimbari vya ya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina.
Habari ID: 3479394 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/09/07
Maelewano ya kidini
IQNA - Wakati wa safari yake katika nchi kubwa zaidi ya Waislamu duniani, Papa Francis alitembelea Msikiti wa Istighlal katika mji mkuu wa Indonesia wa Jakarta siku ya Alhamisi.
Habari ID: 3479389 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/09/06
Wanariadha Waislamu
IQNA – Mwanamke Muirani Sareh Javanmardi wa Iran ameubusu Msahafu (nakala ya Qur'ani Tukufu) baada ya kushinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya Walemavu 2024 huko Paris, hatua ambayo imewavutia Waislamu duniani kote na kupongezwa na taasisi kuu ya Qur'ani.
Habari ID: 3479365 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/09/01
Waislamu Uingereza
IQNA - Takriban mashirika 80 ya Kiislamu na viongozi wa jamii za Waislamu wametoa wito kwa serikali ya Uingereza kuchukua hatua madhubuti ili kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
Habari ID: 3479352 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/30
Arbaeen
IQNA - Mwakilishi wa Jimbo la Utah nchini Marekani Trevor Lee amehimizwa kukutana na Waislamu wa jimbo hilo baada ya video aliyochapisha kusababisha wimbi la chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3479351 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/30
Waislamu Marekani
IQNA - Polisi wa Marekani mjini New York (NYPD) walirarua hijabu za wanawake wengi wa Kiislamu waliokuwa wakiandamana nje ya mkutano wa kukusanya fedha wa Kamati ya Kitaifa ya chama cha Democrat wiki iliyopita.
Habari ID: 3479317 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/23
Waislamu Marekani
IQNA – Baada ya Kongamano la Kitaifa la Chama cha Democrat (DNC) nchini Marekani kukataa kumshirikisha mzungumzaji Mpalestina-Mmarekani katika mkutano wa Chicago, kundi la Waislamu Wanawake Kwa Ajili ya Kamala Harris limetangaza kutumuunga mkono mgombea huyo wa kiti cha rais.
Habari ID: 3479312 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/23
Waislamu Uingereza
IQNA -Kuna wasiwasi unaoongezeka miongoni mwa Waislamu wa Uingereza kuhusu usalama wao baada ya ghasia za hivi majuzi nchini humo.
Habari ID: 3479295 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/18
Dini
IQNA – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei amesisitiza jinsi Waislamu wanavyomheshimu Nabi Isa au Yesu – Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake-(AS), huku akikemea kudhalilishwa kwa mtume huyo Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3479204 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/30
Waislamu Ujerumani
IQNA - Shirika moja lisilo la kiserikali la kimataifa lenye makao yake makuu nchini Iran limelaani vikali marufuku ya Ujerumani dhidi ya Kituo cha Kiislamu cha Hamburg (IZH) na kuitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa wazi wa mikataba ya kimataifa, pamoja na haki za binadamu na uhuru wa dini, kujieleza na kukusanyika.
Habari ID: 3479191 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/27
Waislamu Marekani
IQNA - Mwanaume mmoja katika jimbo la Carolina Kaskazini nchini Markani amekamatwa na kushtakiwa kwa kuvamia na kuharibu msikiti Jumapili jioni.
Habari ID: 3479174 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/23
IQNA - Milio ya risasi karibu na msikiti mmoja nchini Oman kuelekea mkusanyiko wa waombolezaji wa Kishia imesababisha vifo vya takriban watu wanne na kuwaacha wengine kadhaa kujeruhiwa.
Habari ID: 3479135 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/16