qurani tukufu - Ukurasa 17

IQNA

IQNA – Bi Zubaydah Taysert, Waziri wa Utamaduni wa Thailand, alifanya ziara rasmi katika Makumbusho ya Urithi wa Kiislamu na Kituo cha Elimu ya Qur'ani kilichoko katika wilaya ya Yingluck, Jumamosi tarehe 18 Oktoba 2025, kabla ya uzinduzi rasmi wa majengo hayo.
Habari ID: 3481389    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/20

IQNA – Usajili umefunguliwa kwa toleo la 30 la Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikh Jassim bin Muhammad bin Thani nchini Qatar.
Habari ID: 3481388    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/20

IQNA-Katika mji wa Mason, jimbo la Ohio nchini Marekani, kuna shule inayojulikana kama ICM Learning Academy ambayo hufundisha wanafunzi si tu kusoma Qur’ani Tukufu bali pia kuifahamu na kuikumbuka kwa moyo wote.
Habari ID: 3481384    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/19

Ushirikiano katika Qur’ani Tukufu/3
IQNA-Katika Aya ya pili ya Surah Al-Ma’idah, Mwenyezi Mungu Mtukufu ametaja amri nane muhimu, ambazo ni miongoni mwa maagizo ya mwisho aliyoteremshiwa Mtume Muhammad (Rehema na Amani zimshukie). Miongoni mwa amri hizo ni kushikamana kwa pamoja katika njia ya wema na uchamungu.
Habari ID: 3481383    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/19

IQNA-Wizara ya Wakfu wa Kidini ya Misri imemteua rasmi Qari Dkt. Ahmed Ahmed Nuaina kuwa Sheikh al-Qurra, yaani Kiongozi Mkuu wa Wasomaji wa Qur'anI nchini humo.
Habari ID: 3481377    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/17

IQNA – Tarehe 15 Oktoba, katika Msikiti Mkuu wa Astana, Kazakhstan, mashindano ya pili ya Kimataifa ya Usomaji na Kuhifadhi Qur'an Tukufu yamekamilika, yakileta pamoja washiriki 22 kutoka mataifa 21. Tukio hili limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Kiislamu ya Saudi Arabia na Mamlaka ya Kiroho ya Waislamu wa Kazakhstan.
Habari ID: 3481374    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/17

IQNA – Hatua ya mwisho ya Mashindano ya 26 ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind bint Maktoum imeanza rasmi Dubai, ikiwakutanisha wanaume na wanawake wanaohifadhi Qur’ani kutoka kote katika Muungano wa Falme za Kiarabu.
Habari ID: 3481372    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/15

IQNA – Kijana mmoja wa Kipalestina amegundua nakala ya Msahafu ikiwa salama kabisa chini ya magofu ya nyumba yake iliyoharibiwa kaskazini mwa Gaza, akieleza hisia za kina na shukrani baada ya miezi ya mashambulizi.
Habari ID: 3481371    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/15

Ushirikiano katika Qur’ani Tukufu (Sehemu ya Pili)/2
IQNA – Neno Ta’avun (ushirikiano) hutumika kama istilahi ya kielimu katika fani nyingi, lakini katika Seerah ya Mtume Mtukufu (SAW), mara nyingi linahusiana na vitendo vinavyolenga kutimiza mahitaji ya wengine.
Habari ID: 3481365    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/14

IQNA – Mashindano ya kwanza ya Qur'ani na Sunnah yameanza rasmi nchini Brazil, katika bara la Amerika ya Kusini.
Habari ID: 3481364    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13

IQNA – Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yatafanyika wakati wa toleo la pili la Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Libya, yatakayofanyika mjini Tripoli mwishoni mwa mwezi huu.
Habari ID: 3481363    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13

Ushirikiano katika Qur'ani Tukufu/1
IQNA – Uislamu umeamuru wafuasi wake kusaidiana katika kutenda mema. Wakati watu wanapokusanyika na kuanzisha mahusiano ya kijamii, roho ya umoja huingia katika mahusiano yao, na hivyo hujikinga dhidi ya mgawanyiko na kutengana.
Habari ID: 3481360    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13

IQNA – Morocco imezindua jukwaa la kwanza la kidijitali lenye akili mnemba (AI) kwa ajili ya mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu, likilenga kubadilisha kabisa namna mashindano haya yanavyoandaliwa na kusimamiwa.
Habari ID: 3481358    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/12

IQNA – Hukumu dhidi ya mwanaume aliyepigwa faini kwa kuchoma nakala ya Qur'an nje ya ubalozi wa Uturuki jijini London imebatilishwa kwa kisingizio cha eti “uhuru wa kujieleza.”
Habari ID: 3481354    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/11

IQNA – Mradi wa kitaifa uitwao Miqraat al-Majlis (Usomaji wa Kikao) umezinduliwa nchini Misri kwa lengo la kusahihisha usomaji wa Qur'an Tukufu.
Habari ID: 3481351    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/11

IQNA – Baada ya kufanikisha toleo la kwanza la mashindano ya Qur'ani ya ‘Zayin al-Aswat’ nchini Iran, waandaaji wamepanga kuongeza makundi mapya katika tukio hili mashuhuri.
Habari ID: 3481348    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/10

IQNA – Mtaalamu wa chuo kikuu mjini Mashhad nchini Iran amesema kuwa Qur'ani inatoa mwongozo wa kivitendo na wa kimaadili kusaidia jamii kukabiliana na misukosuko kama vile vita, uhamaji, na umasikini.
Habari ID: 3481347    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/10

IQNA – Baraza la Sayansi ya Qur’ani Tukufu linalohusiana na usimamizi wa haram ya Hazrat Abbas (AS) limezindua kozi ya tatu ya mafunzo kwa wasomaji wa kimataifa wa Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3481344    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/08

IQNA – Maonesho ya kimataifa ya Qur’ani yenye mwingiliano wa kisasa, yaliyopewa jina la “Ulimwengu wa Qur’ani”, yamehitimishwa rasmi mjini Kazan nchini Russia au Urusi mnamo Oktoba 6, baada ya kuyazunguka miji ya Moscow, Saratov, na Saransk.
Habari ID: 3481342    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/08

IQNA – Serikali ya Algeria imetangaza kuwa zaidi ya wanafunzi 900,000 wamejiandikisha katika shule za Qur’ani na Zawiya, ikieleza mafanikio makubwa katika mashindano ya kimataifa ya usomaji wa Qur’ani na juhudi zilizopanuliwa za kielimu.
Habari ID: 3481341    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/08