qurani tukufu - Ukurasa 20

IQNA

IQNA-Wizara ya Wakfu wa Kidini ya Misri imemteua rasmi Qari Dkt. Ahmed Ahmed Nuaina kuwa Sheikh al-Qurra, yaani Kiongozi Mkuu wa Wasomaji wa Qur'anI nchini humo.
Habari ID: 3481377   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/17

IQNA – Tarehe 15 Oktoba, katika Msikiti Mkuu wa Astana, Kazakhstan, mashindano ya pili ya Kimataifa ya Usomaji na Kuhifadhi Qur'an Tukufu yamekamilika, yakileta pamoja washiriki 22 kutoka mataifa 21. Tukio hili limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Kiislamu ya Saudi Arabia na Mamlaka ya Kiroho ya Waislamu wa Kazakhstan.
Habari ID: 3481374   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/17

IQNA – Hatua ya mwisho ya Mashindano ya 26 ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind bint Maktoum imeanza rasmi Dubai, ikiwakutanisha wanaume na wanawake wanaohifadhi Qur’ani kutoka kote katika Muungano wa Falme za Kiarabu.
Habari ID: 3481372   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/15

IQNA – Kijana mmoja wa Kipalestina amegundua nakala ya Msahafu ikiwa salama kabisa chini ya magofu ya nyumba yake iliyoharibiwa kaskazini mwa Gaza, akieleza hisia za kina na shukrani baada ya miezi ya mashambulizi.
Habari ID: 3481371   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/15

Ushirikiano katika Qur’ani Tukufu (Sehemu ya Pili)/2
IQNA – Neno Ta’avun (ushirikiano) hutumika kama istilahi ya kielimu katika fani nyingi, lakini katika Seerah ya Mtume Mtukufu (SAW), mara nyingi linahusiana na vitendo vinavyolenga kutimiza mahitaji ya wengine.
Habari ID: 3481365   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/14

IQNA – Mashindano ya kwanza ya Qur'ani na Sunnah yameanza rasmi nchini Brazil, katika bara la Amerika ya Kusini.
Habari ID: 3481364   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13

IQNA – Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yatafanyika wakati wa toleo la pili la Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Libya, yatakayofanyika mjini Tripoli mwishoni mwa mwezi huu.
Habari ID: 3481363   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13

Ushirikiano katika Qur'ani Tukufu/1
IQNA – Uislamu umeamuru wafuasi wake kusaidiana katika kutenda mema. Wakati watu wanapokusanyika na kuanzisha mahusiano ya kijamii, roho ya umoja huingia katika mahusiano yao, na hivyo hujikinga dhidi ya mgawanyiko na kutengana.
Habari ID: 3481360   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13

IQNA – Morocco imezindua jukwaa la kwanza la kidijitali lenye akili mnemba (AI) kwa ajili ya mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu, likilenga kubadilisha kabisa namna mashindano haya yanavyoandaliwa na kusimamiwa.
Habari ID: 3481358   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/12

IQNA – Hukumu dhidi ya mwanaume aliyepigwa faini kwa kuchoma nakala ya Qur'an nje ya ubalozi wa Uturuki jijini London imebatilishwa kwa kisingizio cha eti “uhuru wa kujieleza.”
Habari ID: 3481354   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/11

IQNA – Mradi wa kitaifa uitwao Miqraat al-Majlis (Usomaji wa Kikao) umezinduliwa nchini Misri kwa lengo la kusahihisha usomaji wa Qur'an Tukufu.
Habari ID: 3481351   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/11

IQNA – Baada ya kufanikisha toleo la kwanza la mashindano ya Qur'ani ya ‘Zayin al-Aswat’ nchini Iran, waandaaji wamepanga kuongeza makundi mapya katika tukio hili mashuhuri.
Habari ID: 3481348   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/10

IQNA – Mtaalamu wa chuo kikuu mjini Mashhad nchini Iran amesema kuwa Qur'ani inatoa mwongozo wa kivitendo na wa kimaadili kusaidia jamii kukabiliana na misukosuko kama vile vita, uhamaji, na umasikini.
Habari ID: 3481347   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/10

IQNA – Baraza la Sayansi ya Qur’ani Tukufu linalohusiana na usimamizi wa haram ya Hazrat Abbas (AS) limezindua kozi ya tatu ya mafunzo kwa wasomaji wa kimataifa wa Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3481344   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/08

IQNA – Maonesho ya kimataifa ya Qur’ani yenye mwingiliano wa kisasa, yaliyopewa jina la “Ulimwengu wa Qur’ani”, yamehitimishwa rasmi mjini Kazan nchini Russia au Urusi mnamo Oktoba 6, baada ya kuyazunguka miji ya Moscow, Saratov, na Saransk.
Habari ID: 3481342   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/08

IQNA – Serikali ya Algeria imetangaza kuwa zaidi ya wanafunzi 900,000 wamejiandikisha katika shule za Qur’ani na Zawiya, ikieleza mafanikio makubwa katika mashindano ya kimataifa ya usomaji wa Qur’ani na juhudi zilizopanuliwa za kielimu.
Habari ID: 3481341   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/08

IQNA – Mahakama ya rufaa nchini Sweden (Uswidi) imesitisha hukumu dhidi ya Rasmus Paludan, mwanasiasa wa mrengo wa kulia mwenye uraia wa Denmark na Sweden, ambaye amewahi kutukana na kuchoma nakala za Qur'an Tukufu mara kadhaa.
Habari ID: 3481338   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/07

IQNA – Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametaja Qur’ani Tukufu kuwa silaha yenye nguvu dhidi ya maadui.
Habari ID: 3481333   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/05

IQNA-Katika hafla ya kusisimua iliyofanyika Sa’ada, Yemen, watoto wa mashujaa wameenziwa kwa mafanikio yao katika mashindano ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu, yaliyoandaliwa na Shule ya Qur’ani ya Mashujaa kwa ushirikiano na Taasisi ya Mashujaa.
Habari ID: 3481330   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/05

IQNA – Afisa wa kamati ya maandalizi ya mashindano ya kwanza ya Qur'ani ya Zayin al-Aswat amesema kuwa lengo kuu la tukio hilo la Qur'an ni kutambua, kulea, na kuandaa vipaji mahiri vya vijana kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Habari ID: 3481328   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/04