Abdul Amir Al-Shammari alitoa taarifa hiyo Ijumaa alipokuwa akizuru Mkoa wa Najaf, kusini mwa Iraq.
Amebainisha umuhimu wa mkoa huu katika ibada ya Arbaeen akisema kuwa wakati wa Arbaeen, mamilioni ya wafanyaziyara huingia Najaf, ambao unajulikana kama njia kuu ya wafanyaziyara kuelekea katika tukio hili muhimu.
Al-Shammari ameongeza kuwa vikosi vya uokoaji, timu za ulinzi wa kiraia na huduma za afya katika Najaf ziko tayari kikamilifu.
“Zaidi ya hapo, vikosi vya usalama kutoka mikoa mingine pia vimeingia Najaf ili kutoa msaada,” amesema.
Amesema mpango wa usalama wa ziyara na matembezi ya Arbaeen unatekelezwa vizuri, na idadi ya wafanyaziyara wanaoelekea Karbala inaendelea kuongezeka.
Kuhusu usalama wa barabarani, amesema mpango wa kutenganisha njia za watembea kwa miguu na magari umewekwa ili kuzuia ajali.
Waziri huyo wa mambo ya ndani wa Iraq ameuelezea mpango wa mwaka huu wa usafiri kama bora zaidi kuliko miaka iliyopita, akisema: “Alhamdulillāh, idadi ya ajali za barabarani katika njia za wafanyaziyara imepungua, na ajali zilizotokea katika miaka iliyopita na katika mikoa yote hazijajirudia.”
Amehitimisha kwa kubainisha kuwa usakinishaji wa kamera za uangalizi na rada mpya, doria barabarani, pamoja na utayari kamili wa Idara Kuu ya Trafiki, kumeleta matokeo chanya sana, akisisitiza kuwa wote wanashirikiana kama seli moja, na juhudi kubwa zinafanyika katika nyanja zote ili kuhakikisha usalama na amani.
Arbaeen ni tukio la kidini linalosherehekewa na Waislamu wa Shia siku ya arobaini baada ya siku ya ‘Ashura, kuadhimisha kuuawa shahidi Imam Ḥusayn (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imamu wa tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Ni miongoni mwa mijumuiko mikubwa zaidi duniani ya kila kila mwaka, ambapo mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, pamoja na masunni na wafuasi wa dini nyengine, hutembea kwa miguu kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arubaini itakuwa tarehe 14 Agosti.
3494169