iqna

IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wa Hija
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma kimaendeleo nchi za Kiislamu na akasisitiza kuwa, eneo lote la Kiislamu ni uwanja wa kusimama kifua mbele muqawama kukabiliana na ukhabithi wa Marekani na washirika wake.
Habari ID: 3474113    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/19

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema, uhusiano na ushirikiano imara baina ya Chuo cha Kidini cha Qum na cha Al Azhar cha Misri unaweza kuwa na matokeo chanya na yenye faida kwa Waislamu duniani katika kupambana na ukufurishaji na misimamo ya kufurutu mpaka.
Habari ID: 3474107    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/17

TEHRAN (IQNA)- Iran na Marekani hatimaye zitafikia mapatano ya nyuklia, amesema mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha George Washington.
Habari ID: 3474099    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/14

TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) Ismail Haniya na Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina Ziad al Nakhala wamempongeza rais mteule wa Iran Sayyid Ebrahim Raeisi kwa ushindi wake katika uchaguzi wa rais.
Habari ID: 3474098    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/14

TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema mauaji ya Waislamu wa katika mji wa Srebrenica ni ukurasa mchafu katika historia ya mwanadamu wa leo.
Habari ID: 3474094    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/12

TEHRAN (IQNA)- Rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai amepongeza mazungumzo ya amani baina ya serikali ya Afghanistan na ujumbe wa wanamgambo wa Taliban ambayo yamefanyika wiki iliyopita Tehran.
Habari ID: 3474089    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/10

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Palestina kutokana na kufariki dunia Katibu Mkuu wa Kamandi Kuu ya Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina (PFLP—GC), Ahmad Jibril.
Habari ID: 3474083    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/09

TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Iran ameikosoa vikali Marekani kwa kutoomba radhi kwa kuitungua ndege ya abiria ya Jamhuri ya Kiislamu mwaka 1988 katika Ghuba ya Uajemi na kusisitiza kuwa, Washington inapaswa kubebeshwa dhima kwa kumuenzi kamanda aliyetenda jinai hiyo.
Habari ID: 3474066    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/03

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Redio na Televisheni za Kiislamu amehutubu amsema hatua ya Marekani kufunga tovuti kadhaa za televisheni wanachama wa jumuiya hiyo ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa maoni.
Habari ID: 3474053    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/29

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amesema kuwa wananchi wa Iran ndio washindi halisi wa uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi huu katika mazingira ya maambukizi ya corona na matatizo ya kiuchumi na kwamba wamemfanya adui na vibaraka wake washindwe na kufeli.
Habari ID: 3474049    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/28

Kamanda Mkuu wa IRGC
TEHRAN (IQNA)- Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mafanikio ya Iran katika uga wa sayansi yametokana na kutegemea mantiki ya Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3474046    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/27

TEHRAN (IQNA)- Nasser Abu Sharif, mwakilishi wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina mjini Tehran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni muungaji mkono mkubwa zaidi wa harakati za kupigania ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3474045    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/26

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo Ijumaa hapa mjini amedungwa dozi ya kwanza kabisa ya chanjo ya corona ya COVIran Barekat na kusema kuwa: Kuna ulazima wa kuthamini na kuenzi fahari hii ya taifa ya kuzalisha chanjo ya Ki iran i ya corona.
Habari ID: 3474041    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/25

TEHRAN (IQNA)- Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) limetoa taarifa na kulaani hatua ya tovuti zake kadhaa na za mrengo wa muqawama kufungwa na serikali ya Marekani na kusema kitendo hicho ni ukiukwaji wa wazi wa uhuru wa maoni na ni hujuma dhidi ya vyombo huru vya habari.
Habari ID: 3474036    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/23

TEHRAN (IQNA)- Kumekuwa na ongezeko la asilimi 20 la Misahafu iliyochapishwa nchini Iran katika mwaka huu wa Ki iran i wa Hijria Shamsia ulioanza Machi 21.
Habari ID: 3474034    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/23

TEHRAN (IQNA) – Kiongozi mwandamizi wa Kiislamu nchini Iraq Sayyid Muqtada al Sadr ametoa wito kwa Iran na Saudi Arabia kutatua hitilafu zao kupitia mazungumzo.
Habari ID: 3474031    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/22

TEHRAN (IQNA)- Tuko katika kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ridha AS, mmoja kati ya Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 3474029    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/21

TEHRAN (IQNA)- Rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumza na waandishi habari kuhusu sera za kitaifa na za kimataifa za serikali yake
Habari ID: 3474027    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/21

TEHRAN (IQNA) - Viongozi mbali mbali duniani wanaendelea kumtumia salamu za pongezi Sayyid Ebrahim Raeisi kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanyika Ijumaa.
Habari ID: 3474024    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/20

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyed Hassan Nasrallah amempongeza Sayyid Ebrahim Raeisi kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanyika Ijumaa.
Habari ID: 3474023    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/20