
Akizungumza katika mahojiano na IQNA, Anfal Al-Hilw alisema kuwa Iran imehakikisha kuwa ile fikra ya istiqamah na uthabiti imeondoka katika ngazi ya nara na kauli mbiu na kufika katika utekelezaji, kupitia Muqawama au mapambano katika ulimwengu wa Kiarabu
Amesema kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yalibadilika kuwa mradi wa kimahesabu katika wa kijamii uliovuka mipaka ya taifa pale yalipokuwa yakionyesha mfano mpya wa uhuru wa kisiasa na kitamaduni, ukizingatia kupinga udhibiti wa kigeni na kulinda heshima ya mataifa.
“Mfano huu, ulioegemea kwenye uhusiano kati ya utambulisho wa Kiislamu na uamuzi huru, ulihamasisha mataifa huru na harakati za kanda, na hatimaye kuunda mhimili wa Muqawama kama mfumo wa pamoja wa kukabiliana na miradi ya kikoloni na Kizayoni.”
Alipohojiwa kuhusu uhusiano kati ya Mapinduzi ya Kiislamu na suala la Palestina, alisema kuwa uhusiano huo ni wa msingi na wa lazima, kiasi kwamba tangu mwanzo wa ushindi wa mapinduzi, Palestina ilitambulishwa kama kipaumbele cha kati katika dunia ya Kiislamu.
“Uhusiano huu unaonekana wazi leo katika msaada wa kisiasa, kiroho, na vyombo vya habari kwa watu wa Palestina, na katika mjadala unaoona ukombozi wa Palestina kama sehemu ya mradi mkubwa wa ukombozi kutoka kwa ukoloni na udhibiti, hasa kuhusiana na maendeleo katika Gaza na maeneo mengine ya Palestina.”
Kuhusu uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kubadilisha mlingano wa nguvu za kikanda dhidi ya mradi wa Magharibi-Kizayuni kwa kuunga mkono mhimili wa Muqawama, Al-Hilw alisema kuwa msaada wa Iran umeleta mabadiliko yanayoshikika katika usawa wa nguvu za kikanda, kiasi kwamba sera haziundwi tena kwa hiari ya pande moja ya Magharibi na utawala wa Kizayuni.
3496308