IQNA

Al Houthi: Marekani na Israel zinajaribu kutekeleza njama dhidi ya Waislamu

11:49 - February 03, 2022
Habari ID: 3474884
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Marekani na utawala haramu wa Israel ni maadui nambari moja wa Waislamu duniani.

Akizungumza Jumanne  wakati wa mkutano na wawakilishi wa makabila kutoka maeneo yote ya Yemen, Sayyid Abdul-Malik al-Houthi amesema tawala za Marekani na Israel zinajaribu kutekeleza njama dhidi ya Waislamu kwa kutumia hitilafu zilizopo ndani ya umma wa Waislamu duniani.

Aidha amesema utawala haramu wa Israel na mamluki wake wanalitazama taifa la Yemen kama adui. Abdul Malik Al Houthi ameashiria hatua ya baadhi ya nchi za Kiarbau kuingia katika mkataba unaoungwa mkono na Marekani wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusema nchi hizo za Kiarabu sasa zinatekeleza sera zinazoenda sambamba na utawala huo haramu.

Ameendelea kusema, ni wazi sasa kuwa Umoja wa Falme za Kiarbau, utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia zimechukua muelekeo wa pamoja wa uhasama dhidi ya taifa la Yemen.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ikishirikiana na UAE na kwa himaya ya Mareakni na utawala haramu wa Israel na madola mengine ya Magharibi ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha usukani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh.

Vita vilivyoanzishwa  na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Yemen na kuendelea hadi sasa vimeshapelekea mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia kupoteza maisha, mbali na kuwaacha mamilioni wakiwa hawana pa kuishi. Aidha vita hivyo vimesababisha matatizo mengi ya ukosefu wa chakula, matibabu na elimu kwa watu wa Yemen.

Katika kulipiza kisasi jinai hizo, Jeshi la Yemen hutekeleza mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya maeneo ya kistratijia ya Saudi Arabia na UAE.

4033189

captcha