IQNA

Muqawama

Kiongozi wa Ansarullah: Hatua ya maadui kuua viongozi wa muqawama hazitutetereshi hata kidogo

11:51 - August 02, 2024
Habari ID: 3479211
IQNA- Kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, katika kipindi cha miaka yote hii, wakuu wa Kambi ya Muqawama wamethibitisha kwamba, jinai zinazofanywa na maadui haziwatetereshi hata kidogo, bali zinaongeza tu ari na moyo wao wa Jihadi na Muqawama.

Abdul Malik al Houthi ameyasema hayo katika hotuba yake ya kila wiki aliyoitoa jana Alkhamisi na kusisitiza kuwa, jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel hivi sasa ni ishara ya kukaribia kuangamia utawala huo dhalimu akisisitiza kuwa, kadiri jinai hizo zinavyoongezeka ni kwa kiwango hichocho ndivyo zinavyoifanya thabiti na imara zaidi imani ya wanajihadi na wanamapambano katika kambi ya Muqawama.

Wakati huo huo tovuti ya televisheni ya Al Masirah ya Yemen imezungumzia jinai ya Israel ya kumuua shahidi Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS na kusema kuwa huo ndio mwisho bora na uliojaa baraka wa wanamapambano wa Kiislamu na watu walio imara katika njia ya Allah.

Amma kuhusiana na jinai nyingine ya Israel ya kumuua shahidi Fuad Ali Shukr, mmoja wa makamanda wa Hizbullah ya Lebanon na mauaji ya wanamapambano kadhaa ya harakati ya ukombozi ya wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi katika shambulio la Marekani mkoani Babel huko Iraq, Abdul Malik al Houthi amesema kuwa, kuuawa shahidi katika njia ya Haki ni sehemu ya maisha ya viongozi na makamanda wa Muqawama na kwamba kwa jinai zake hizo utawala wa Kizayuni wa Israel umejisogeza karibu zaidi na maangamizi yake kama inavyosema ahadi ya Allah.

4229595

captcha