Ripoti zinaeleza kuwa, kwa mara nyingine tena mamilioni ya wananchi wa Yemen walimiminika barabarani kulaani jinai za utawala wa Kizayuni na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina hasa wa Ukanda wa Gaza.
Mbali na San'a mikoa mingine kulikofanyika maandamano makubwa ya wananchi wa Yemen ni pamoja na Hudaydah, Sa'ada, Ma'rib na mikoa mengine kama ya Umran, Aab, Taiz, Dhamar, n.k.
Mkoa wa Hudaydah ulishuhudia maandamano 66 katika mji mkuu wa mkoa huo na wilaya na mikoa yote, chini ya kauli mbiu "Wito wa Maulid ya Mtume wa kuunga mkono Al-Aqsa na Gaza".
Viwanja vyote vilijaa umati mkubwa wa watu ili kuendana na sherehe za Maulid au kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), ambapo waliimba qasida za mapenzi kwa tukio kubwa na takatifu zaidi katika historia.
Washiriki hao wamelaani jinai zinazoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watoto na wanawake wa Gaza, uvamizi wa wazayuni hao dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa na jinai nyingine ya askari wa Kizayuni ya kurarua nakala za Qur'ani Tukufu na katika msikiti wa Ukanda wa Gaza hivi karibuni.
Taarifa iliyotolewa na mikutano ya hadhara ilisisitiza kuendelea kwa maandamano ya kila wiki hadi ushindi, Mwenyezi Mungu akipenda, kuhuisha ahadi na utiifu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na kuendelea katika njia ya jihad na kuunga mkono Wapalestina hasa wa Gaza..
Kauli hiyo pia ilihuisha ahadi kwamba watu wa Hudaydah na Wayemeni wengine wataitetea Al-Aqsa katika mji wa Quds na kubaki imara katika msimamo wao wenye kanuni wa kuwaunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa.
3489785