IQNA

Maulidi

Waethiopia washiriki sherehe kubwa  Milad-un-Nabi nchi nzima

15:51 - September 17, 2024
Habari ID: 3479448
IQNA – Waislamu nchini Ethiopia walisherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume (SAW) kwa sherehe za kidini kote nchini.

Waislamu wa Ethiopia walisherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) kwa sherehe mbalimbali kote katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, maelfu ya Waislamu walikusanyika Jumamosi jioni kwenye Msikiti wa Grand Anwar pamoja na viongozi wa kidini kusherehekea tukio hilo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pia alitoa salamu za heri kwa watu wa Ethiopia katika ujumbe wake Jumamosi usiku, kuadhimisha sherehe za kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), sherehe ambazo ni maarufu kama Maulidi au Milad un Nabii

Katika ujumbe wake, Waziri Mkuu alisema kuwa kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) ni fursa ya kutafakari lengo letu la maisha. Aliongeza kuwa ni wakati wa kufikiria juu ya malengo yake na kutafakari ujumbe wake ambao umekuwa na athari kubwa kwa ulimwengu.

Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa nchini Ethiopia kwa idadi ya wafuasi, ikiwa na wastani wa Waislamu milioni 35 nchini humo.

Nchini Ethiopia, kama ilivyo katika nchi nyingine zenye idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni, mazazi ya Mtume (SAW) huadhimishwa tarehe 12 Rabi' al-Awwal.

4236963

Habari zinazohusiana
captcha