
Mohammad Reza Jafarpour alitwaa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Hifdh ya Qurani Tukufu yote, huku Mehdi Rashtbari akipata nafasi ya pili katika kipengele cha usomaji (tilawa) wa Qur'ani.
Hatua ya mwisho ya mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani ilifanyika kwa ana kwa ana mjini Beirut tarehe 13 na 14 Februari, baada ya hatua za awali kufanyika kwa njia ya mtandao.
Mashindano hayo yaliandaliwa na Kituo cha Kitamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, kwa ushirikiano na Jumuiya ya Qur'ani Tukufu ya Lebanon.
Jopo la majaji lilijumuisha wanazuoni na wataalamu mashuhuri wa Qur'ani, akiwemo Hujjatul Islam Mohammad Haji Abolqasem na Ali Mehrabi kutoka Iran; Adel Khalil, Sheikh Mohammad Al‑Saleh na Haitham Ayyash kutoka Lebanon; Sheikh Khairuddin Al‑Hadi kutoka Iraq; Kamal Qada kutoka Algeria; pamoja na Sheikh Abdel Nasser Harak kutoka Misri.
Kwa mujibu wa vigezo vya majaji, katika kipengele cha usomaji wa Qur'ani, tathmini ilijumuisha:
Katika kipengele cha Hifdh, vigezo vilikuwa:
Ushindi huu unaakisi kiwango cha juu cha taaluma ya Qurani miongoni mwa washiriki wa Iran, na unaimarisha nafasi ya mashindano haya kama jukwaa muhimu la kukuza uhusiano wa Qurani na mshikamano wa kiroho miongoni mwa Waislamu wa mataifa mbalimbali.
3496431