Hujjatul Islam Seyed Mehdi Khamoushi aliyasema hayo katika kikao cha Makao Makuu ya Uratibu wa Mashindano ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kilichofanyika Jumatano mjini Tehran.
Mkutano huo ulioandaliwa kwa ajili ya kujadili kuandaliwa kwa duru ya mwisho ya Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran na Mashindano ya 41 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran, ulihudhuriwa pia na Hamid Majidimehr, Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Shirika la Wakfu, Shobeyr Firouzian, Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu anayesimamia masuala ya Qur'ani na Etrat, na maafisa wengine wa Qur'ani ncini Iran.
Hujjatul Islam Seyed Mehdi Khamoushi ameyataja mashindano ya Qur’ani ya Iran kuwa fahari kwa mrengo wa muqawama katika ulimwengu wa Kiislamu unaopambana na madola ya kibeberu.
Amebainisha kuwa mji mtakatifu wa Mashhad utakuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya kimataifa mwaka huu, akitumai kuwa yatafungua ukurasa mpya wa kuandaa hafla hiyo ya kifahari.
Kwingineko katika kikao hicho, Majidimehr aliwasilisha ripoti kuhusu maandalizi ya kuandaa matukio hayo mawili ya Qur'ani, na kubainisha kwamba duru ya mwisho ya Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran itafanyika katika mji wa Tabriz kaskazini magharibi mwa nchi hiyo kuanzia tarehe 2 hadi 19 Disemba.
4250949