IQNA

Waziri wa Wakfu Algeria Abainisha Mafanikio Katika Kufundisha Qur’ani

22:55 - January 05, 2025
Habari ID: 3480007
IQNA - Waziri wa Masuala ya Dini na Wakfu wa Algeria amesisitiza mafanikio ya nchi hiyo katika sekta ya elimu ya Qur’ani.

Sheikh Youcef Belmehdi ameeleza kuwa Algeria imechukua hatua kubwa kuboresha elimu ya Qur’ani na kutumia zana na teknolojia za kisasa kufundisha Kitabu cha Mungu. Alikuwa akizungumza wakati wa ziara katika vituo kadhaa vya Qur’ani na vituo vya kidini katika Mkoa wa Naama, al-Masa iliripoti. Amesisitiza juhudi za serikali kuunga mkono na kupanua taasisi za elimu ya Qur’ani, shule za kidini, na Maktab (shule za jadi za Qur’ani) ili kuunda mazingira ya kiroho, kuendeleza tabia za Kiislamu, na kuwasilisha elimu na kuhudumia Qur’ani.

Belmehdi alibainisha kuwa idadi ya wanafunzi katika vituo vya elimu ya Qur’ani imepita milioni 1.2 ya wavulana na wasichana, na alisisitiza msaada wa maafisa wa ngazi za juu wa nchi hiyo kwa maendeleo ya mfumo wa elimu ya Qur’ani. Alisema pia wizara inashughulika na elimu ya Qur’ani katika ngazi ya vyuo vikuu, kuhamasisha wanafunzi wa Qur’ani, kuandaa mipango ya usomaji wa serikali, na kugundua wasomaji bora na wenye sifa kupitia matukio na mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ya kuhifadhi, kusoma, na kutoa tafsiri ya Qur’ani.

Afisa huyo wa Algeria amesisitiza jukumu la maimamu wa misikiti katika kukuza uelewa miongoni mwa vizazi ili kuhifadhi taifa, kujivunia mafanikio, na kuthamini maadili ya kihistoria na kidini. Amesema  ni tafakari kuona watu wa Algeria wana dhamira na azma a kudumia maadili yao ya kitaifa ya kidini.

Aliendelea kusema kuwa misikiti inaendelea kuwa na jukumu muhimu katika kuimarisha maadili ya kitamaduni na kidini, pamoja na kuendeleza mshikamano wa kijamii, wakati mashirika ya elimu ya hisani pia yana jukumu kubwa katika juhudi hizi.

3491328/

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu algeria
captcha