IQNA

Hamas: Kwa kila Shahidi, Mwenge wa Muqawama  unawake zaidi

21:28 - March 23, 2025
Habari ID: 3480421
IQNA – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Palestina Hamas ililaani mauaji ya Salah al-Badrawil yaliyofanywa na utawala katili wa Israel, ikisisitiza kuwa kwa kila shahidi, mwenge wa Muqawama unazidi kuwa mkali.

Jeshi la utawala haramu wa Israel lilifanya mashambulizi mapya ya angani ya kikatili katika Ukanda wa Gaza, likiwa limeua jumla ya watu 40, wakiwemo al-Bardawil, mbunge wa Palestina na mwanachama wa ofisi ya kisiasa ya Hamas.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, Hamas ilisema Bardawil alilengwa katika operesheni ya "mauaji ya kikatili ya Kizayuni," akiwa katika ibada ya swala ya usiku wa 23 wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Bardawil, iliongeza, aliuawa pamoja na mke wake katika shambulio la anga la Israel lililolenga hema lake katika eneo la al-Mawasi, magharibi mwa jiji la Khan Yunis la Gaza kusini. Hamas pia imemuenziBardawil kama "nembo ya kazi ya kisiasa, vyombo vya habari, na kitaifa," ikibainisha kuwa "hakushindwa kamwe kutekeleza wajibu wake au … jihad (jitihada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu)" yenye lengo la kuendeleza malengo ya Palestina. Hamas imesisitiza kuwa utawala wa kihalifu wa Israel hautadhoofisha uthabiti na uvumilivu wa Wapalestina kwani "kwa kila shahidi, mwenge wa mwenge wa Muqawama unazidi kuimarika na mkali hadi uvamizi utakapomalizika."

3492475

captcha