Kamati ya Uratibu wa Hatua za Pamoja kwa Palestina nchini Tunisia iliandaa maandamano hayo kwa jina la "Siku ya Kitaifa Tunisia ya Kuharamisha Uhusiano na Israel". Maandamano jijini Tunis yalianzia Bab al-Khazra Square na kugeuka kuwa mkutano wa kupinga mbele ya bunge katika wilaya ya Bardo.
Miji mingine ya Tunisia, kama Gafsa, Gabes, na Tataouine, pia ilishuhudia maandamano kama hayo. Waandamanaji walipaza sauti wakitaka uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni kupigwa marufuku nchini Tunisia.
Pia wametoa wito wa kufukuzwa kwa balozi wa Marekani nchini Tunisia, kukomesha uhusiano wa kijeshi na kiusalama na Washington, na kususia kampuni zinazounga mkono uvamizi wa utawala haramu wa Israel.
Maandamano hayo yalifanyika wakati utawala wa Israeli ukiendelea na vita vya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza. Kulingana na ripoti ya Economist, utawala huo unalenga kuangamiza kabisa Gaza, ikiwa ni sehemu ya mpango mpana wa kulazimisha zaidi ya wakazi milioni mbili wa Gaza kuondoka kwenye eneo hilo la Palestina.
3492658