IQNA

Tishio la shambulio kwa Msikiti wa Brisbane laibua malalamiko ya Waislamu duniani

15:15 - May 12, 2026
Habari ID: 3482230
IQNA – Tishio la mtu mmoja la kufyatua risasi dhidi ya waumini katika msikiti mmoja mjini Brisbane, Australia, limeibua malalmiko duniani kutoa ambapo shirika mashuhuri la haki za kiraia la Waislamu nchini Marekani limetoa tamko rasmi.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) siku ya Jumatatu lilieleza mshikamano wake na jamii ya Waislamu wa Australia baada ya mtu mmoja kutishia kuwashambulia waumini katika msikiti ulioko Brisbane.

Inaelezwa kuwa waumini katika Msikiti wa Taqwa mjini Brisbane walitishiwa na mtu aliyeingia ndani ya jengo hilo na kudai kuwa alikuwa na silaha nje ya msikiti huo, tukio lililotokea Jumapili asubuhi. Baadaye polisi walimtafuta na kumkamata mshukiwa, ambaye alishtakiwa kwa makosa ya kusababisha usumbufu kwa umma na kuvuruga utulivu wa mahali pa ibada. Mnamo mwezi Desemba, msikiti huo pia uliharibiwa kwa kuchorwa alama ya Kinazi ya swastika na maandishi ya chuki dhidi ya Waislamu.

“Tunasimama kwa mshikamano na ndugu zetu Waislamu nchini Australia, na tunawashukuru maafisa wa usalama kwa kuchukua hatua za haraka na kumkamata mshukiwa,” alisema Ismail Allison, Meneja wa Mawasiliano wa Kitaifa wa CAIR. “Chuki ya vurugu dhidi ya Waislamu ni tishio kwa jamii za Kiislamu popote duniani na ni lazima ipingwe kila inapojitokeza.”

Aliongeza kuwa hapo awali CAIR pia ilionyesha mshikamano na raia wa Australia waliokuwa wakipinga ziara ya Rais wa Israel Isaac Herzog, baada ya polisi kuwanyanyasa waandamanaji na kuwazuia kwa nguvu baadhi ya Waislamu kutekeleza ibada ya swala.

Mnamo mwezi Januari, CAIR pia ilitoa tamko la mshikamano na jamii ya Waislamu nchini Australia kufuatia taarifa za shambulio la chuki lililomlenga Imamu (kiongozi wa kidini) pamoja na mkewe.

Mwaka uliopita, CAIR iliungana na Waislamu wa Australia kulaani shambulio la kifo lililolenga jamii ya Kiyahudi nchini humo, na pia ikamsifu Mwislamu mmoja aliyesifiwa kama “shujaa” kwa kuchukua hatua ya kumpokonya silaha mmoja wa washambuliaji.

3497426

captcha