IQNA

‘Kitendo Kisichokubalika’: Umoja wa Mataifa walaani jinsi Israel ilivowatendea wanaharakati wa Msafara wa Meli za Gaza

10:29 - May 22, 2026
Habari ID: 3482270
IQNA – Umoja wa Mataifa umelaani jinsi Israel ilivyowatendea wanaharakati waliokuwa katika meli za misaada zilizoelekea Gaza baada ya msafara huo kukamatwa katika maji ya kimataifa.

Ofisi ya Haki za Binadamu ya UN siku ya Alhamisi imesema kuwa video ya tukio hilo ni “ya kuudhi kupita kiasi” na ikatoa wasiwasi kuhusu uwezekano wa kukamatwa na kuzuiliwa kinyume cha sheria katika maji ya kimataifa.

“Kile kinachoonekana katika video hii ni cha kushangaza na cha kuudhi,” msemaji Ravina Shamdasani amesema katika taarifa.

Alikuwa akirejea video iliyoshirikiwa na waziri mwenye misimamo mikali katika utawala wa Israel, Itamar Ben‑Gvir, inayoonyesha wanaharakati waliokamatwa wakiwa wamefungwa kwa  mikononi na kulazimishwa kupiga magoti baada ya kukamatwa na askari katili  wa Israel katika maji ya kimataifa.

Msafara wa meli za misaada wa Global Sumud ulisema Jumanne kwamba meli zote 50 za msafara wake zilitekwa na Israel baada ya kushambuliwa katika maji ya kimataifa katika kitendo ambacho kimetajwa kuwa ni uharamia wa kiserikali.

Shamdasani amesema ofisi yake “ina wasiwasi mkubwa juu ya hali inayowakumba mamia ya wanaharakati walioelekea Gaza waliokamatwa na vikosi vya Israel wakiwa ndani ya meli zenye bendera za kigeni katika maji ya kimataifa, na kisha kushikiliwa na jeshi la majini la Israel, kufuatia kile kinachoonekana kuwa ni kukamatwa na kuzuiliwa kinyume cha sheria.”

Amesema kuwa kutangaza kuwa kosa kutoa msaada wa kuokoa maisha ni “jambo lisilokubalika kabisa.”

3497551

captcha