marekani - Ukurasa 2

IQNA

IQNA-Rais wa Iran, amehoji katika ujumbe aliouelekeza kwa wananchi wa Marekani kwamba: Vita vinavyoendelea sasa vinanufaisha vipi maslahi halisi ya watu wa Marekani? Amesisitiza kuwa mashambulio dhidi ya miundombinu muhimu ya Iran, ikiwemo vituo vya nishati na viwanda, ni hatua inayolenga moja kwa moja kuvuruga maisha ya watu wa Iran.
Habari ID: 3482113    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/02

IQNA – Kitendo cha mtu mmoja kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu katika msikiti mmoja huko Brooklyn, Marekani  kimezua lawama kali, huku polisi wa New York (NYPD) wakichunguza tukio hilo kama uhalifu wa chuki.
Habari ID: 3482105    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/30

IQNA-Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) limelaani shambulio la Marekani na Israel dhidi ya Shule ya Shajareh Tayyebeh katika mji wa Minab, kusini mwa Iran, ambapo angalau wanafunzi na wafanyakazi wa shule 175 waliuawa katika mauaji ya kikatili tarehe 28 Februari.
Habari ID: 3482097    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/28

IQNA-Jeshi la Yemen limetangaza kuwa liko tayari kuingilia moja kwa moja kijeshi iwapo pande nyingine zitaungana na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Mhimili wa Muqawama.
Habari ID: 3482096    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/28

IQNA-Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema mauaji ya wanafunzi katika Shule ya Minab yaliyotekelezwa na Marekani na Israel ni “sehemu ndogo tu ,” ya jinai ya kivita unaofanywa na muungano huo wa kijeshi wa tawala hizo mbili.
Habari ID: 3482095    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/28

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani/4
IQNA-Katika matukio ya hivi karibuni, mbele ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kulikuwepo njia mbili: vita au mazungumzo. Watu wengi kwa kawaida walipendelea mazungumzo. Hata hivyo, kwa nini hatima ya nchi ikaishia kwenye vita?
Habari ID: 3482033    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/09

IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu vitisho vya mara kwa mara vya kijeshi kutoka Marekani dhidi ya Iran, akisema kuwa silaha zenye uwezo wa kuzamisha manowari za Marekani ni “hatari zaidi” kuliko meli hizo za kivita zenyewe.
Habari ID: 3481951    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/17

IQNA-Kiongozi wa harakati ya Muqawama (mapambano ya Kiislamu) ya Ansarullah nchini Yemen amesema kuwa Marekani na Utawala wa Israel zinakabiliana na Iran kwa sababu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasimama kama kizuizi dhidi ya mradi wao mpana wa kutawala eneo la Asia Magharibi au Mashariki ya Kati.
Habari ID: 3481932    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/14

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameonya kwamba, vita vyovyote vitakavyoanzishwa na Marekani dhidi ya Iran vitageuka na kuwa vita vya kikanda.
Habari ID: 3481877    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/01

IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema Marekani ilichochea machafuko ya hivi karibuni nchini Iran, na kwamba imefedheheka kwani njama za zimepata kipigo kikubwa cha kimkakati.
Habari ID: 3481834    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/23

IQNA – Baraza la Mashauriano la Mashirika ya Kiislamu Malaysia (MAPIM) limetoa tamko likieleza kuunga mkono msimamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kuhusu kumweka rais wa Marekani kuwa na dhima juu ya vifo na uharibifu uliotokana na machafuko ya hivi karibuni nchini Iran.
Habari ID: 3481821    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/19

IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema Iran inamtambua Rais wa Marekani, Donald Trump, kama mhusika mkuu wa mauaji na uharibifu katika ghasia za hivi karibuni hapa nchini.
Habari ID: 3481813    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/18

Wizara ya Mambo ya Nje imelaani vikali tamko la hivi karibuni la kuingilia mambo ya ndani ya Iran lililotolewa na Kundi la Nchi Saba (G7), ikilishutumu kundi hilo la kiserikali linaloongozwa na Marekani kwa kuingilia masuala ya Iran na kwa mtazamo wa kinafiki kuhusu haki za binadamu.
Habari ID: 3481812    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/17

IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuhusika moja kwa moja Marekani, utawala wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Ulaya katika matukio ya hivi karibuni ya Iran hakukanushiki.
Habari ID: 3481809    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/17

IQNA-Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amezionya Marekani, Israel na mamluki wao wenye mienendo ya kigaidi kama ile ya Daesh kwamba kosa lolote la kimahesabu litakabiliwa na majibu makali na ya kuangamiza.
Habari ID: 3481805    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/15

QNA – Mwanasiasa mmoja wa Marekani ameonya kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika nchi za Magharibi wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani unakaribia.
Habari ID: 3481802    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/14

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kundi la watu waharibifu Alhamisi usiku mjini Tehran waliharibu mali za umma na za wananchi kwa ajili ya kumfurahisha rais wa Marekani huku akisisitiza kuwa Iran haitalegeza msimamo katika kukabiliana na magenge ya wahalifu.
Habari ID: 3481785    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/10

IQNA – Katika hatua ya kutambua historia na mchango wa Waislamu wake, Jimbo la New York limetangaza mwezi wa Januari kuwa Mwezi wa Urithi wa Waislamu wa Marekani.
Habari ID: 3481778    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/07

IQNA – Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina, qari mashuhuri wa Misri, amechapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook video inayoonyesha mwanamke M marekani akisilimu katika moja ya misikiti nchini Marekani.
Habari ID: 3481769    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/05

IQNA – Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon imesisitiza katika taarifa yake kwamba watu wa Venezuela, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, watazima njama ya Marekani. Wameongeza kuwa mataifa huru na yenye mamlaka yao yanapaswa kusimama pamoja kukabiliana na dhulma na jinai za Marekani na kuunda ushirikiano wa kimkakati.
Habari ID: 3481767    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/05