imam khamenei - Ukurasa 2

IQNA

IQNA-Baraza Kuu la Usalama wa Taifa limetoa taarifa kuhusu ushindi wa kihistoria wa Iran katika vita vya tatu vilivyolazimishwa dhidi yake, pamoja na kukubaliwa kwa masharti ya Iran na upande wa adui.
Habari ID: 3482126    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/08

IQNA – Baadhi ya wanazuoni na maqari mashuhuri wa Qur’ani Tukufu kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu katika siku za karibuni wametangaza msimamo wao wa kulaani vikali uvamizi ulioanzishwa na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3482123    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/07

IQNA – Qari wa Qur’ani Tukufu kutoka Kuwait ameunga  mkono shambulio vita haramu vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuibua hasira kubwa na ukosoaji kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Habari ID: 3482115    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/03

IQNA-Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limetungua ndege ya pili ya kisasa ya Marekani aina ya F-35 ikiwa katika anga katikati ya Iran kwa kutumia mfumo mpya wa ulinzi wa anga wa Kikosi cha Anga cha jeshi hilo.
Habari ID: 3482114    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/03

IQNA-Rais wa Iran, amehoji katika ujumbe aliouelekeza kwa wananchi wa Marekani kwamba: Vita vinavyoendelea sasa vinanufaisha vipi maslahi halisi ya watu wa Marekani? Amesisitiza kuwa mashambulio dhidi ya miundombinu muhimu ya Iran, ikiwemo vituo vya nishati na viwanda, ni hatua inayolenga moja kwa moja kuvuruga maisha ya watu wa Iran.
Habari ID: 3482113    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/02

IQNA – Kadiri vita vya kichokozi vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran vinavyoendelea, bendera ya rangi tatu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ishara ya wazi ya Muqawama au mapambano na ya iradaya pamoja ya wananchi, walioungana zaidi katika nyakati ngumu.
Habari ID: 3482112    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/01

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ametoa shukrani kwa wanazuoni wa Kisuni katika Mkoa wa Kurdistan nchini Iran kufuatia ujumbe wao wa pole na mshikamano baada ya kuuawa shahidi aliyekuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Habari ID: 3482109    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/01

IQNA – Qari mashuhuri kutoka Pakistan, Mohammad Davoud, amejiunga na kampeni ya Qur’ani iitwayo “Kuelekea Fath (Ushindi) wa Utawala wa Faqihi Mtawala.”
Habari ID: 3482106    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/30

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshukuru na kuthamini misimamo ya msingi ya wanazuoni wakuu wa kidini na wananchi wa Iraq.
Habari ID: 3482104    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/30

IQNA – Taasisi ya Qur’ani ya Yemen iitwayo “Noon” imeukosoa msimamo wa hivi karibuni wa Kituo cha Kiislamu cha Al‑Azhar cha Misri dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ikisema kuwa unakinzana na wito wa Qur’ani Tukufu wa kusimama upande was haki na uadilifu.
Habari ID: 3482100    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/28

IQNA-Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) limelaani shambulio la Marekani na Israel dhidi ya Shule ya Shajareh Tayyebeh katika mji wa Minab, kusini mwa Iran, ambapo angalau wanafunzi na wafanyakazi wa shule 175 waliuawa katika mauaji ya kikatili tarehe 28 Februari.
Habari ID: 3482097    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/28

IQNA-Jeshi la Yemen limetangaza kuwa liko tayari kuingilia moja kwa moja kijeshi iwapo pande nyingine zitaungana na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Mhimili wa Muqawama.
Habari ID: 3482096    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/28

IQNA-Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema mauaji ya wanafunzi katika Shule ya Minab yaliyotekelezwa na Marekani na Israel ni “sehemu ndogo tu ,” ya jinai ya kivita unaofanywa na muungano huo wa kijeshi wa tawala hizo mbili.
Habari ID: 3482095    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/28

Rais wa Iran katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Malaysia
IQNA-Rais wa Iran amesema katika mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Malaysia kwamba nchi za Kiislamu hazipaswi kuwaruhusu maadui kupanda mbegu za mifarakano na kuwasha moto wa vita.
Habari ID: 3482094    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/27

IQNA – Kituo cha Kiislamu cha AlAzhar nchini Misri kimehimizwa kufikiria upya msimamo wake kuhusu mashambulizi yanayoendelea ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, na pia kutafakari kwa makini kuhusu mustakabali wa ulimwengu wa Kiislamu na Umma wa Waislamu.
Habari ID: 3482090    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/26

IQNA – Sayyid Ammar al‑Hakim, kiongozi wa Harakati ya Hikma ya Kitaifa ya Iraq, amelaani vikali shambulio la Marekani dhidi ya makao makuu ya Vikosi vya Kujitolea vya Umma (PMU) katika jimbo la Anbar.
Habari ID: 3482088    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/25

IQNA – Iran ni nchi ambayo viongozi, maafisa wa serikali na makamanda wa kijeshi hawasimami kutoa heshima kwa majeneza ya wanajeshi wao; badala yake mara nyingi wao hutangulia kuuawa shahidi, kisha wananchi wa nchi yao ndio huwapa mazishi na kuwaaga kwa heshima.
Habari ID: 3482087    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/25

IQNA-Mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu nchini Kenya, Shakira Wafula, ametangaza mshikamano wake na watu wa Iran na Palestina, akitoa ujumbe wa imani na matumaini.
Habari ID: 3482085    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/24

IQNA-Mufti Mkuu wa Libya ametoa taarifa kuhusu mashambulizi na uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kwa mara nyingine amesisitiza kuwa: Ni wajibu kuwahami Waislamu pale vita vinapotokea baina ya Waislamu na makafiri.
Habari ID: 3482084    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/24

IQNA – Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo amekosoa vikali vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, akivitaja kuwa ni fedheha kwa familia nzima ya kibinadamu na mtihani mkubwa wa maadili kwa ulimwengu mzima.
Habari ID: 3482082    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/23