IQNA

Iran yatungua ndege ya pili ya kivita ya Marekani aina ya F-35

19:17 - April 03, 2026
Habari ID: 3482114
IQNA-Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limetungua ndege ya pili ya kisasa ya Marekani aina ya F-35 ikiwa katika anga katikati ya Iran kwa kutumia mfumo mpya wa ulinzi wa anga wa Kikosi cha Anga cha jeshi hilo.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) mapema Ijumaa (Aprili 5), imesema kwamba ndege ya pili ya kivita ya Marekani aina ya F-35, kutoka Kikosi cha Laken-Heath, imepigwa na kusambaratishwa katika anga ya kati ya Iran kwa kutumia mfumo mpya wa kisasa wa ulinzi wa anga wa IRGC.

Kwa mujibu wa taarifa ya IRGC, ndege hiyo ya kivita imeharibiwa kabisa na kuanguka. Hii ni ndege ya pili ya kivita kutunguliwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa IRGC katika kipindi cha masaa kumi na mbili. Ndege nyingine aina ya F15 imetuna imetunguliwa ndani ya anga ya Iran na marobani wake wawili bado hawajulikani waliko. Operesheni ya Marekani ya kujaribu kuwaokoa marubani hao imefeli baada ya helikipota iliyokuwa ikitumiwa nayo pia kuripotiwa kulengwa.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetangaza kwamba hakujapatikana taarifa kuhusu hatima ya rubani wa ndege hiyo ya kivita ya Marekani kutokana na kuharibiwa kikamilifu kwa sababu ya mlipuko mkali uliotokana na kupigwa kombora na kisha kuangakua chini. Taarifa hiyo inasema uwezekano kwamba rubani wake ameokoka shambulizi hilo ni mdogo.

Kutunguliwa ndege hiyo ya kisasa zaidi ya Marekani katika anga ya Iran kunakuja baada ya madai ya uongo ya rais kidhabi wa nchi hiyo, Donad Trump, kwamba ulinzi wa anga wa Iran umeharibiwa kabisa.

Kabla ya hapo ndege ya kivita ya Marekani pia ilipigwa kusini mwa Kisiwa cha Qeshm (kusini mwa Iran) na kuangukia katika maji ya Ghuba ya Uajemi.

4344094

captcha