iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Watu wa Iraq wameandamana katika mji mkuu, Baghdad, kulaan kitendo cha kigaidi cha Marekani cha kuwaua makamanda wakuu wa vita dhidi ya ugaidi, Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na mwanamapmabano mwenza wa Iraq Abu Mahdi al Muhandis.
Habari ID: 3473496    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/27

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon
TEHRAN (IQNA) - Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Shahidi Qassem Soleimani alikuwa nguvu kubwa mbele ya mipango kiistikbari ya Marekani na ndio maana ameuliwa kigaidi na adui.
Habari ID: 3473480    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/22

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wauaji wa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani lazima walipiziwe kisasi na kisasi hiki hakina shaka na kitatekelezwa wakati wowote.
Habari ID: 3473463    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/16

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema hakuna chembe ya shaka kwamba Iran italipiza kisasi cha kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC.
Habari ID: 3473185    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/19

Kwa mara ya kwanza duniani
TEHRAN (IQNA) - Kwa mara ya kwanza duniani, Jamhuri ya Kislamu ya Iran imevumbua kifaa chenye uwezo wa kugundua mwili na sehemu kilipo kirusi cha corona katika umbali wa mita 100 tena katika kipindi cha sekunde chache tu. Kifaa hicho kimepewa jina la "Musta'an 110."
Habari ID: 3472670    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/16

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu asema
TEHRAN (IQNA) - Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amemtaja Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC kama shakhsia aliyehuisha 'harakati za jihadi na kuuawa shahidi' katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3472471    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/14

TEHRAN (IQNA) - Marasimu ya maombolezo ya arubaini ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) yamefanyika Alhamisi kote nchini Iran kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa matabaka mbalimbali ya wananchi.
Habari ID: 3472469    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/14

TEHRAN (IQNA)- Kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuwaunga mkono Wapalestina na kuhakikisha kuwa ndoto zao za kuwa taifa huru zinafanikiwa.
Habari ID: 3472433    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/02

TEHRAN (IQNA) - Mwakilishi maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran ametoa matamshi ambayo yanashiria utambulisho wa kigaidi wa serikali ya Washington ambapo amezungumza kuhusu kumuua kamanda aliyechukua nafasi ya kamanda Muirani Shahidi Luteni Jenerali Qasem Soleimani.
Habari ID: 3472399    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/23

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
THERAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pigo la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kwa adhama ya Marekani ni jambo ambalo limepelekea nchi hiyo ifedheheke na kuongeza kuwa: "Pigo hilo kubwa na lenye nguvu haliwezi kufidiwa kwa chochote na hivyo hatua ya hivi karibuni ya Marekani ya kuongeza vikwazo haiwezi kuondoa fedheha hiyo."
Habari ID: 3472379    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/17

TEHRAN (IQNA) – Wananchi wa Nigeria wamendamana kulaani jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Habari ID: 3472332    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/04

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kutokana na kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Suleimani na kusema kuwa: Kisasi kikali kinawasubiri watenda jinai ambao mikono yao michafu imemwaga damu yake na mashahidi wengine katika shambulizi la usiku wa kuamkia leo.
Habari ID: 3472329    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/03

TEHRAN (IQNA) - Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Luteni Jenerali Qassem Suleimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes wameuawa shahidi mapema leo Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika barabara ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
Habari ID: 3472328    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/03

Kamanda Mkuu wa IRGC
TEHRAN (IQNA)- Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) mezungumzia mwamko na muono wa mbali wa wananchi wa Iran katika matukio ya hivi karibuni humu nchini na kusisitiza kuwa, wiki zilizopita, wananchi wa Iran walitoa pigo jingine kubwa kwa mabeberu hususan Marekani.
Habari ID: 3472256    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/04

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), amesisitiza kwamba maadui wamefikia mwisho wa njia na kwamba licha ya haiba yao ya kidhahiri lakini mifupa yao imeoza kwa ndani.
Habari ID: 3471961    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/05/17

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani inahasimiana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kwa sababu jeshi hilo limekuwa mstari wa mbele katika kuilinda Iran na Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: "Kwa miaka 40 sasa, Marekani na maadui wengine wajinga wamekuwa wakifanya kila wawezalo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lakini wameshindwa."
Habari ID: 3471906    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/09

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kuhitimishwa satwa ya mti khabithi wa kundi la kigaidi la ISIS ni pigo kwa serikali za huko nyuma na za sasa za Marekani pamoja na tawala vibaraka na tegemezi kwa Washington katika Mashariki ya Kati ambazo zililianzisha kundi hili na kuliunga mkono kwa hali na mali ili zitanue satwa zao katika eneo hili na hivyo kuufanya utawala ghasibu wa Israel uwe na udhibiti wa eneo hili.
Habari ID: 3471274    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/11/22