IQNA

Binti Muirani mwenye ulemavu wa macho kuwakilisha Iran mashindano ya Qur’ani kimataifa

20:23 - November 30, 2021
Habari ID: 3474623
TEHRAN (IQNA)- Zahra Khalili, msichana mwenye ulemavu wa macho katika mji mkuu wa Iran, Tehran ni miongoni mwa wawakilishi wanne wa Iran katika mashindano yajayo ya Qur’ani ya kimataifa ya wanafunzi Waislamu.

Anatazamiwa kushiriki katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu katika kitengo cha wasichana.

Naye Maryam Sabzevari kutoka mkoa wa Khuzestan ataiwakilisha Iran katika kategoria ya qiraa katika mashidano hayo.

Kwa upande wa wavulana Iran itawakilishwa na Muhammad Reza Jafarpour wa mkoa wa Gilan na Amir Ali Yadegar wa  mkoa wa Tehran katika kategoria za kuhifadhi na qiraa kwa taratibu.

Wanafunzi wote hao wamechaguliwa kufuatia mashindano ya kitaifa ya Qur’ani ya wanafunzo yaliyofanyika katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Duruy ya 7 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanafunzi itafanyika Tehran baina ya Februari na Machi 2022.

3476726

captcha