IQNA

Qur'ani Tukufu katika Maisha

Kongamano la Kuala Lumpur kujadili Qur’ani Tukufu inavyoweza kutatua changamoto za kisasa

20:38 - December 02, 2022
Habari ID: 3476185
TEHRAN (IQNA) - Kongamano limepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Malaysia Disemba 3 kujadili masuluhisho ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za siku hizi.

Taasisi ya Warisan Ummah Ikhlas Foundation (WUIF) ndiyo inayoandaa hafla hiyo kwa kushirikisha wataalamu kutoka nchi kadhaa.

Wazungumzaji watatoka Malaysia, Indonesia, Bangladesh, Misri, Marekani na Palestina.

Ukumbi wa Perdana MTI huko Kuala Lumpur utaandaa mjumuiko huo ambapo washiriki watajadili ujumbe wa Sura As-Sajdah na masuluhisho inayotoa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha itakuwa mada kuu ya kongamano hilo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Marhaini Yusoff, watu wanakabiliwa na changamoto nne leo, ambazo ni za kifedha, kazi, familia na kijamii au kiroho na wanahitaji kukabiliana na changamoto hizo kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.

Ameongeza kuwa taasisi hiyo imeandaa hafla hiyo ya kimataifa ili kujaribu kutafuta njia za kukabiliana na changamoto za maisha kwa kuzingatia mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

WUIF pia kila mwaka hupanga Malaysia #QuranHour, tukio linalolenga kuleta jamii za Waislamu karibu na Qur’ani Tukufu kupitia usomaji na ufahamu wa kina wa aya zake.

  4103923

Kishikizo: malaysia ، qurani tukufu ، kisasa
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha