Zaidi ya wafanyaziara 15,000 walinufaika na programu hizi, ambazo ziliendelea hadi mwisho wa mwezi wa Hijri wa Safar (Septemba 4), idara hiyo imetangaza.
Matukio hayo ya Qur'ani, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wanawake ya Shughuli za Qur'ani, inayofungamana na idara hiyo, yalijumuisha vipindi vya usomaji Qur'ani na kampeni ya kurekebisha makosa katika usomaji.
Minar al-Jabouri, mkuu wa taasisi hiyo, alisema pia kulikuwa na shughuli za kitamaduni na kidini, zikiwemo ibada za maombolezo, kujibu maswali ya kidini, kutoa huduma za matibabu, afya na nyinginezo.
Alisema hema maalum lililopewa jina la Hadhrat Ruqayyah (SA) pia liliwekwa ambamo programu za Qur'ani zilifanyika kwa ajili ya watoto.
Ameongeza kuwa, wanawake kutoka sehemu mbalimbali za dunia hukutana wakati wa ibada ya Ziyara na matembezi ya Arbaeen, ambayo inatoa fursa kwa ajili ya kuongeza ufahamu na kukuza utamaduni wa Qur'ani na kanuni za harakati ya Imam Hussein (AS).
Wakati wa msimu wa Arbaeen, taasisi hiyo ilianzisha vituo 17 vya Qur'ani katika barabara zinazoelekea Karbala ili kuandaa programu za Qur'ani na kutoa huduma za Qur'ani, kitamaduni na kidini kwa mahujaji wa kike.
Arbaeen ni tukio la kidini linaloadhimishwa na Waislamu, hasa wa madhehebu ya Shia, katika siku ya arobaini baada ya Siku ya Ashura, kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na imamu wa tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Ni miongoni mwa safari kubwa zaidi za kila mwaka duniani, huku mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wakitembea kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen iliangukia tarehe 25 Agosti.
3489773