Katika visa 3,866 vilivyoripotiwa kwa mwaka moja kuanzia Machi 2023 hadi Machi 2024, Waislamu ndio kundi lililoathiriwa zaidi. Takwimu hizo, zilizotolewa siku ya Alhamisi, pia zinaonyesha ongezeko la asilimia 25 la uhalifu wa chuki za kidini ikilinganishwa na mwaka uliopita, na hivyo kuashiria ongezeko kubwa zaidi ya kila mwaka tangu rekodi zilipoanza mwaka 2012.
Ghasia za mrengo wa kulia na hali mbaya ya kisiasa imechangia kuhalalisha chuki dhidi ya Uislamu. Mwenendo huu umechangiwa na matamshi ya kisiasa yenye migawanyiko ambayo yanaendelea kuzinyanyapaa jamii za Kiislamu. Kuongezeka kwa mashambulizi na ubaguzi kunaonyesha jinsi chuki dhid ya Uislamu ilivyo katika jamii ya Uingereza, Baraza la Waislamu la Uingereza (MCB) limebainisha katika taarifa yake ya Ijumaa.
Akijibu data hizo za hivi punde, Katibu Mkuu wa MCB Zara Mohammed alisema, "Ongezeko la uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu, kwa kusikitisha, halishangazi na ishara ya namna kushadidi ubaguzi na uhasama dhidi ya Waislamu wa Uingereza."
Aliongeza, "Tumeona matamshi ya kisiasa yenye kuibua mifarakano ambayo yanaendelea kuzinyanyapaa jumuiya za Kiislamu kwa manufaa ya kisiasa, pamoja na habari za uongo zinazochochea ghasia za mrengo mkali wa kulia na mashambulizi yanayochochewa na chuki dhidi Uislamu, zinazoonyesha jinsi masuala haya yalivyozama."
Mohammed pia alidokeza kuwa uhalifu mwingi wa chuki wenye chuki dhidi ya Uislamu hauripotiwi, akionyesha kuwa data hiyo inaangazia sehemu ndogo tu ya suala hilo na sio asili yake ya kimfumo.
Ripoti hiyo pia inasisitiza kimuundo chuki dhidi ya Uislamu katika taasisi zote muhimu kama vile mamlaka za mitaa na mashirika ya serikali, ambayo inazidisha ukosefu wa usawa.
Waislamu wa Uingereza wanakabiliwa na vikwazo vikubwa katika kupata huduma za afya, nyumba, na ajira kutokana na upendeleo wa kitaasisi, ilisema MCB, ikiongeza kuwa hii inajenga hali ya uhasama ambapo chuki dhidi ya Uislamu inaendelezwa sio tu kupitia vitendo vya mtu binafsi bali pia na mifumo inayokusudiwa kuwalinda raia.
MCB inaitaka serikali kutimiza wajibu wake wa kulinda jamii zote dhidi ya chuki, kushughulikia ongezeko la ugaidi wa mrengo mkali wa kulia, na kukabiliana na kukita kitaasisi chuki dhidi ya Uislamu.
3490225