Sheikh Naim Qassem amemhutubu tena Shahidi Nasrullah na kusema: "njia ya Hizbullah iliundwa kwa fikra zako, nafsi yako na damu yako, na Palestina ilipandwa ndani ya nyoyo zetu."
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameendelea kumhutubu Shahidi Nasrullah na kusema: "njia yako, Ewe Nasrullah, ni ya milele. Ni kweli kwamba waliulenga mwili wako, lakini roho yako ingali iko hai".
Akimhutubu tena Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Shahidi Safiyyuddin, Katibu Mkuu mwingine wa Hizbullah aliyeuawa shahidi huko Lebanon, Sheikh Naim Qassem alisema: "mumeondoka mapema sana na kutuacha, lakini athari zenu zinaendelea kubaki, na sisi tuaendelea kuheshimu na kutimiza ahadi tuliyotoa kwenu".
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Sheikh Naim Qassem ameendelea kusema: "tulisimama imara dhidi ya vita vya kimataifa ambapo utawala wa Kizayuni ulijaribu kuufuta Muqawama ili kufungua njia ya kuundwa 'Israel Kubwa'".
Amekumbusha kwa kusema: "baada ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kuuawa shahidi makamanda wa Muqawama, maadui walidhani tutaporomoka, lakini kwa kuchaguliwa makamanda wapya wa Hizbullah, tuliweza kudhibiti tena hatamu za uendeshaji wa mambo."
Kuhusiana na njama ya kutaka kuupokonya silaha Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema: "Marekani na utawala wa Kizayuni ni hatari kwa Lebanon na Muqawama, na sisi hatutaruhusu katu Muqawama upokonywe silaha na tutakabiliana nao katika vita vya Kikarbala."
Sheikh Naim Qassem ametuma pia salamu kwa wananchi, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akisema: "kwa uungaji mkono wao, wamewezesha Muqawama kuendelea kubaki kwenye mkondo wake."
Aidha amesema: "tunatuma salamu zetu kwa Yemen, ambayo imegharimika sana kwa ajili ya kuendelea kubaki heshima na adhama ya Muqawama".
Katibu Mkuu wa Hizbullah amewahutubu pia wafuasi wa harakati hiyo ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon akisema: "tutaendelea kuheshimu na kutimiza ahadi yetu na tutaendeleza njia ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah".
3494773