IQNA

Kiongozi wa Kisunni Iran: Umoja wa Waislamu utavunja njama za maadui

12:01 - February 17, 2026
Habari ID: 3481950
IQNA – Mwanazuoni wa Kisunni kutoka Iran amesema kuwa kulinda umoja wa Umma wa Kiislamu kutazima njama zote zinazopangwa na maadui.

Maulawi Nazir Ahmad Salami, mwakilishi wa wananchi wa mkoa Sistan na Baluchestan katika Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kusimamia kazi zake  (Majlis-e Khobregan), amesema kuwa jambo linalowatia hofu kubwa zaidi maadui ni umoja na mshikamano wa Umma wa Kiislamu neema kubwa ambayo, endapo itahifadhiwa, itaweza kubatilisha mipango na njama nyingi.

Akirejelea maendeleo ya hivi karibuni katika eneo hilo, alisema kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, makosa na uhalifu mkubwa umetendeka nchini Palestina, ambao kwa mtazamo wa maoni ya umma duniani umefichua wazi ukatili na kutokuwa na huruma kwa wahusika, na kwa kiwango kikubwa zaidi umeonyesha sura halisi ya wale wanaodai kutetea haki za binadamu.

Alisisitiza kuwa lengo kuu la maadui ni kuinyima Umma wa Kiislamu amani na usalama kwa kupanda mbegu za mifarakano na migawanyiko.

“Maadui wanajaribu kufikia malengo yao kwa kuleta mgawanyiko na kudhoofisha mshikamano, ilhali Umma wa Kiislamu una neema kubwa za kimada na kiroho ambazo, endapo zitatumika ipasavyo, zinaweza kufungua njia ya heshima, maendeleo na ustawi,” alisema.

4334673

captcha