IQNA

Qur’ani Tukufu yavunjiwa heshima New York, uchunguzi waanza

20:15 - March 30, 2026
Habari ID: 3482105
IQNA – Kitendo cha mtu mmoja kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu katika msikiti mmoja huko Brooklyn, Marekani  kimezua lawama kali, huku polisi wa New York (NYPD) wakichunguza tukio hilo kama uhalifu wa chuki.

Tawi la New York la Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR‑NY), ambalo ni sehemu ya shirika kubwa zaidi la kutetea haki za kiraia za Waislamu nchini Marekani, siku ya Jumapili kitendo cha kuunajisi msikiti mmoja wa Brooklyn kwa kinyesi pamoja na kupatikana kurasa zilizochanwa za Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama, mshukiwa aliulenga msikiti wa Islamic Mission of America ulioko Brooklyn Heights kwa kurusha kurasa za Qur’ani kwenye ngazi za mbele za jengo hilo, kisha akarejea baadaye na kupaka kinyesi mlangoni, kama polisi walivyoeleza. Mshukiwa huyo alivaa kofia nyeusi ya kichwani na barakoa nyeusi iliyokuwa imeshuka chini ya kidevu chake. Tukio hilo lililotokea tarehe 9 Machi linafanyiwa uchunguzi kama uhalifu wa chuki.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa CAIR‑NY,

“Jaribio hili lililoripotiwa la kuidhalilisha Qur’ani Tukufu linatisha sana na linaonyesha wazi chuki iliyolenga nyumba ya ibada. Tunazipongeza mamlaka za usalama kwa kulichunguza tukio hili kama uhalifu wa chuki, na tunasisitiza kufanyika kwa uchunguzi wa haraka na wa kina ili mhusika awajibishwe. Hakuna jamii inayopaswa kuishi kwa hofu ya kunyanyaswa au kushambuliwa kwa sababu ya imani zao za kidini.

Tunathibitisha tena dhamira yetu ya kulinda haki za kiraia na heshima ya kila mtu. Vitendo vya chuki havina nafasi katika jamii yetu, na sote kwa pamoja tunapaswa kuvipinga na kupambana na ubaguzi katika aina zake zote.”

Shirika la CAIR pia hutoa kijitabu kiitwacho “Mbinu Bora za Usalama wa Misikiti na Jamii,” ambacho kinatoa ushauri wa namna ya kusaidia kulinda maeneo ya ibada. Mwongozo huo unaweza kutumika kwa nyumba za ibada za dini zote.

Siku ya Ijumaa, makao makuu ya CAIR yaliyoko Washington, D.C., pamoja na CAIR‑NY, pia yalipokea kwa kuridhika taarifa za kuzuiwa kwa njama ya kulipua kwa moto nyumba ya mwanaharakati wa Kipalestina anayeishi New York, Nerdeen Kiswani.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya haki za kiraia ya CAIR, malalamiko kuhusu chuki na ubaguzi dhidi ya Waislamu yanaendelea kuongezeka kote nchini Marekani, jambo linaloonyesha kuwepo kwa mwenendo unaoendelea wa Chuki Dhidi ya Uislamu (Islamophobia) unaoathiri jamii mbalimbali nchini humo.

3496921/

captcha