IQNA

Mwanazuoni wa Iran Atumia Mantiki ya Qur’ani Kupinga Lobi za Kizayuni

10:54 - April 25, 2026
Habari ID: 3482161
IQNA – Mwanazuoni mashuhuri wa sayansi za hisabati kutoka mji wa Yazd nchini Iran ametoa changamoto ya kielimu kwa lobi za Kizayuni.

Profesa Bijan Davvaz, anayeheshimika kimataifa katika taaluma ya sayansi za hisabati, ametangaza changamoto hiyo ya kielimu na kiteolojia kwa lobi za Kizayuni ulimwenguni, akitumia hoja za kimantiki zenye mizizi katika Qur’ani Tukufu.

Profesa Davvaz, ambaye jina lake limewahi kutajwa miongoni mwa wanasayansi wenye ushawishi mkubwa duniani, anajulikana kwa machapisho yake mengi yaliyorejelewa kwa wingi, vitabu vikuu vya marejeo vya kimataifa, na ushirikiano na watafiti kutoka karibu nchi 40.

Katika ujumbe wake uliolenga lobi za Kizayuni kote duniani, zikiwemo za Marekani, Profesa Davvaz alitoa changamoto mbili mahsusi akirejea aya za Qur’ani Tukufu.

Akinukuu aya za Suratul-Jumu‘ah (62:6) na Suratul-Baqarah (2:94), profesa huyo alieleza kuwa Qur’ani inawapa changamoto wanaodai kuwa wao ni watu wateule wa Mwenyezi Mungu kwa kusema: “Basi tamani kifo ikiwa nyinyi ni wakweli.”

“Kwani mbona mnakimbilia mafichoni kwa khofu ya mauti?” aliuliza moja kwa moja.

Profesa Davvaz pia alieleza kuwa Qur’ani ina ahadi ya Mwenyezi Mungu isiyopingika (Al-Isra, 17:6) kwamba madhalimu wakizidi katika ufisadi na ujeuri, Mwenyezi Mungu atawawekea juu yao watu watakaowaadhibu hapa hapa duniani.

Akinukuu Suratul-Baqarah (2:120) inayosema kwamba Kizayuni “hawataridhika nanyi mpaka mfuate dini yao,” Profesa Davvaz alisema kuwa haiwezekani kufikia mapatano nao.

“Mkakati wenu wa vita, usitishaji vita, kisha mazungumzo, ambao mmeutumia kwa muda mrefu dhidi ya wanaotafuta uhuru duniani, mwishowe utawarejea wenyewe,” aliwaonya, akisisitiza kuwa Qur’ani Tukufu haiwezi kupotoshwa, hata kama watajaribu kufanya hivyo.

Akimuelekea moja kwa moja Rais wa Marekani Donald Trump, profesa huyo alinukuu aya ya Qur’ani inayosema kuwa Mwenyezi Mungu “hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.”

Uzayuni ni itikadi ya kisiasa yenye misingi ya utaifa mkali, ambayo imehusishwa na harakati za ukoloni wa makazi na mizozo ya muda mrefu inayohusisha uvamizi wa kijeshi, unyakuzi wa ardhi, sera za ubaguzi, na mateso dhidi ya Wapalestina katika ardhi za Palestina ambazo zilianza kukaliwa kwa mabavu na utawala bandia wa Israel mwaka 1948.

3497196

Kishikizo: uzayuni qurani tukufu
captcha