waislamu - Ukurasa 50

IQNA

TEHRAN (IQNA) - Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo hufanyika kwa njia ya moja kwa moja kupitia Televisheni ya Al Kauthar ya Iran yameanza.
Habari ID: 3472714   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/29

TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Polisi Afrika Kusini Bheki Cele amewaomba radhi Waislamu nchini humo baada ya afisa wa polisi kutamka matamshi ya kuvunjia heshima Uislamu wakati akiwakamata waumini waliokuwa wamekiuka sheria za kuzuia mijimuiko kutokana na janga la corona.
Habari ID: 3472709   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/27

TEHRAN (IQNA) – Wanamgambo wa jenerali muasi Khalifa Haftar nchini Libya wameushambulia msikiti karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.
Habari ID: 3472708   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/27

TEHRAN (IQNA) – Mwanachama wa Kamati ya Hilali ya Mwezi nchini Iran amesema hilali ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani haitazamiwi kuonekana Alhamisi Aprili 23.
Habari ID: 3472695   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/23

TEHRAN (IQNA)- Ubaguzi wa Waislamu nchini India ambao umeongezeka katika miezi ya hivi karibuni sasa umekithiri zaidi wakati huu wa janga la corona.
Habari ID: 3472690   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/21

TEHRAN (IQNA) –Mhubiri wa Kiislamu Nigeria amekamatwa katika jimbo la Kano kaskazini mwa nchi hiyo baada ya kuswalisha Sala ya Ijumaa kwa siri kinyume cha amri ya serikali.
Habari ID: 3472688   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/21

TEHRAN (IQNA)- Viongozi wanne maarufu wa jamii ya Waislamu nchini Marekani wanachangisha fedha za kuwasiaidia maimamu na wafanyakazi wa misikiti katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa corona au COVID-19 nchini humo.
Habari ID: 3472685   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/20

TEHRAN (IQNA) – Sheria ya kutotoka nje ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona nchini India imepelekea Waislamu wa jamii ya Rohingya wasiweze kupokea msaada wa chakula kutoka kwa wahisani na hivyo wanakabiliwa baa la njaa.
Habari ID: 3472681   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/19

TEHRAN (IQNA) – Shirika la Hilali Nyekundu la Uturuki limetangaza mpango wa kuwasaidia Waislamu 10 nchini Uturuki na maeneo mengine duniani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472674   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/17

TEHRAN (IQNA) - Kufuatia uhaba wa vifaa vya wauhudumu wa afya katika hospitali za Marekani, Waislamu wa nchi hiyo wameunda kundi la kujitolea katika kupambana na virusi vya Corona.
Habari ID: 3472672   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/17

TEHRAN (IQNA) – Wakuu wa Saudi Arabia wako mbioni kuzuia kuenea ugonjwa wa corona au COVID-19 katika mji mtakatifu wa Makka kutokana na kuenea kwa kasi ugonjwa huo mjini humo pamoja na kuwa kunatekeleza sheria ya kutotoka nje kwa masaa 24.
Habari ID: 3472664   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/14

TEHRAN (IQNA) – Idadi kubwa ya Waislamu wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona nchini Uingereza na hilo linabainika wazi katika makaburi ya Waislamu.
Habari ID: 3472658   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/12

TEHRAN (IQNA)- Maimamu na wanafikra kadhaa wa Kiislamu na Kiarabu duniani wametia wametoa wito wa kutaka Zaka itumike katika jitihada za kukabiliana na janga la ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472654   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/11

TEHRAN (IQNA) – Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametoa hakikisho kuwa, Waislamu watakaofariki nchini humo kutokana na ugonjwa wa COVID-19 au corona watazikwa kwa mujibu wa taratibu za Kiislamu.
Habari ID: 3472648   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/09

TEHRAN (IQNA) – Baraza la Maulamaa Russia limetangaza Fatwa mpya inayowataka Waislamu waswali katika majumba yao katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika mwaka huu wa 1441 Hijria Qamaria ili kuzuia kuenea zaidi ugonjwa ambukizi wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472647   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/09

Janga la Corona
TEHRAN (IQNA) – Pakistan imewaweka katika karantini watui 20,000, na inawasaka maelifu yaw engine, walioshiriki katika mjumuiko wa Waislamu ambao ni maarufu kama Ijtimai katika mji wa Lahore mwezi uliopita, huku janga la COVID-19 au corona likiendelea kuwa mbaya nchini humo.
Habari ID: 3472646   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/08

TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Idara ya Hija na Ziyara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea matumaini yake kuwa, janga la COVID-19 au corona litamalizika utakapowadia msimu wa joto na kwamba Hija itafanyika kama ilivyopangwa. Hatahivyo ameongeza kuwa, Iran iko tayari kwa hali yoyote itakayojitokeza kuhusu Ibada ya Hija mwaka huu.
Habari ID: 3472643   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/07

TEHRAN (IQNA) – Makundi ya wabaguzi wenye misimamo mikali wa mrengo wa kulia yanatumia janga la ugonjwa wa COVID-19 au corona kueneza chuki dhidi ya Waislamu nchini Uingereza.
Habari ID: 3472640   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/06

TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu nchin Misri imetangaza kuwa ni marufuku kuandaa futari kwa umma misikitini katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472635   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/05

TEHRAN (IQNA) – Ugonjwa wa COVID-19 au corona umepelekea kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu nchini India.
Habari ID: 3472631   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/04