iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza masikitiko yake kuhusiana na mkasa wa ndege ya abiria ya Ukraine iliyotunguliwa kimakosa karibu na mji wa Tehran ambapo sambamba na kusema kuwa, yuko pamoja na familia zilizopoteza ndugu zao katika mkasa huo wa kuhuzunisha ametoa amri ya kufanyika uchunguzi kuhusiana na uwezekano wa kufanyika uzembe na wahusika kuchukuliwa hatua.
Habari ID: 3472362    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/11

TEHRAN (IQNA) -Khitma kwa mnasaba wa kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wanajihadi wenzake katika hujuma ya kigaidi ya Marekani mefanyika leo hapa Tehran katika Husseiniya ya Imam Khomeini kwa kuhudhuriwa na Kingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei.
Habari ID: 3472355    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/09

TEHRAN (IQNA) – Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limetoa ushauri kwa Wairani-Wamarekani (Wairani wenye uraia wa Marekani) baada ya kubainika kuwa wanasumbuliwa na kubaguliwa na maafisa wa usalama kufuatia matukio ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3472349    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/07

TEHRAN (IQNA) – Shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani amezikwa kwa kuchelewa kufuatia msongamano mkubwa katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa Iran.
Habari ID: 3472347    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/07

TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3472337    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/05

TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani amesema: Jina la Luteni Jenerali Qassem Soleimani litaheshimika na kubakia milele katika historia ya taifa la Iran na wapigania uhuru duniani.
Habari ID: 3472334    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/04

TEHRAN (IQNA) – Wananchi wa Nigeria wamendamana kulaani jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Habari ID: 3472332    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/04

Khatibu wa Sala ya Ijumaa
TEHRAN (IQNA) - Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria juu ya kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusisitiza kuwa, Wamarekani katu hawataonja tena ladha ya amani popote duniani kufuatia ukatili huo.
Habari ID: 3472330    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/03

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kutokana na kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Suleimani na kusema kuwa: Kisasi kikali kinawasubiri watenda jinai ambao mikono yao michafu imemwaga damu yake na mashahidi wengine katika shambulizi la usiku wa kuamkia leo.
Habari ID: 3472329    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/03

TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya watu wa India wameukaribisha mwaka mpya wa 2020 Miladia kwa maandamano ya kupinga sheria ya uraia inayowabagua Waislamu.
Habari ID: 3472327    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/02

TEHRAN (IQNA) – Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad nchini Iraq, Jumatnao ulitangaza kusitisha huduma zote kwa umma kufuatia maandamano ya wananchi waliokuwa na hasira wa Iraq nje ya ubalozi huo.
Habari ID: 3472326    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/02

TEHRAN (IQNA) – Mwanamke Mwislamu nchini Marekani ametimuliwa katika mgahawa aliokuwa akifanya kazi kwa sababu tu ya kuja kazini akiwa amevalia vazi la staha la Hijabu.
Habari ID: 3472325    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/02

TEHRAN (IQNA) – Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina 149 katika mwaka uliopita wa 2019, aghalabu wakiwa katika Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3472322    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/01

TEHRAN (IQNA) – Idara ya Kufuatia Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika Chuo cha Al Azhar nchini Misri imelaani hatua mwanasiasa mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi ya kupanga kufanyika mashindano ya vibonzo vya kumdhalilisha Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 3472321    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/31

TEHRAN (IQNA) - Malefu ya wananchi wenye hasira nchini Iraq leo wameandamana mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad baada ya mazishi ya wapiganaji wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi maarufu kama Al Hashd al Shaabi ambapo wamelaani vikali hujuma ya anga ya Marekani dhidi ya vituo vya harakati hiyo.
Habari ID: 3472320    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/31

TEHRAN (IQNA) –Mkutano mkubwa zaidi ya Waislamu Marekani umefanyika katika mji wa Chicago na kuwaleta pamoja Waislamu zaidi ya 25,000 na wageni waalikuwa kutoka dini zingine.
Habari ID: 3472319    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/31

TEHRAN (IQNA) – Magazeti nchini Uingereza vimekuwa vikiwasilisha taswira mbaya na potovu kuhusu Uislamu na Waislamu.
Habari ID: 3472317    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/30

TEHRAN (IQNA) - Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amepinga kulegeza misimamo mbele ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ajili ya kutoa suhula mbalimbali huko Ghaza mkabala na Hamas kusitisha uvurumishaji wa makombora katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3472316    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/30

TEHRAN (IQNA) – Waislamu wasiopungua 40wameuawa katika mapigano yaliyojiri hivi karibuni huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Habari ID: 3472315    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/30

TEHRAN (IQNA)- Duru ijayo ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran itafanyika katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuanzia siku ya 8 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani inayokadiriwa kuwa Aprili 20.
Habari ID: 3472314    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/29