qurani tukufu - Ukurasa 6

IQNA

IQNA – Mafanikio ya kihistoria katika sanaa ya hati za Kiislamu yamezinduliwa mjini Istanbul: Ni nakala kubwa zaidi ya Qur'ani duniani iliyoandikwa kwa mkono, matokeo ya juhudi za miaka sita bila kukata tamaa.
Habari ID: 3481436    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/29

IQNA – Jumuiya ya Qur'ani Tukufu ya Mauritania imetangaza uzinduzi wa kampeni ya kusambaza nakala 50,000 za Qurani nchini humo.
Habari ID: 3481434    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/29

IQNA – Mkuu wa Taasisi ya Wakfu na Misaada ya Iran ameielezea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ndiyo kinara wa kukuza Qur’ani Tukufu katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3481432    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/28

Ushirikiano Katika Qur’ani Tukufu/6
IQNA – Mbali na ukweli kwamba mali kwa asili ni ya Mwenyezi Mungu ambaye ameikabidhi kwa mwanadamu, utajiri wa asili pia ni haki ya wanajamii wote, kwani rasilimali hizi ziliumbwa kwa ajili ya watu wote, si kwa ajili ya mtu binafsi au kikundi maalum.
Habari ID: 3481431    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/28

IQNA – Kamati ya maandalizi ya Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran imetangaza rasmi majina ya washindi wa tukio hilo mashuhuri la Kiqur’ani.
Habari ID: 3481429    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/28

IQNA – Mfungwa wa Kipalestina aliyeachiwa hivi karibuni amefichua mambo manne muhimu yanayochangia kuenea kwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika Ukanda wa Gaza, licha ya mzingiro, vita na uharibifu.
Habari ID: 3481424    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/27

IQNA – Mfungwa wa Kipalestina aliyeachiliwa kutoka gereza la utawala wa Kizayuni ameeleza mateso makali na hali isiyo ya kibinadamu inayowakumba wafungwa wa Kiislamu, ikiwemo udhalilishaji wa Qur'an Tukufu na kuzuia adhana na sala za jamaa.
Habari ID: 3481418    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/26

Ushirikiano katika Qur’ani Tukufu/5
IQNA – Kwa mujibu wa mtazamo wa Kiislamu, binadamu wote ni waja wa Mwenyezi Mungu, na mali yote ni ya Mwenyezi Mungu. Hivyo basi, mahitaji ya wale wasiojiweza yanapaswa kutimizwa kupitia ushirikiano wa kijamii.
Habari ID: 3481415    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/25

IQNA – Usajili umefunguliwa rasmi kwa toleo la 21 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Algeria, mojawapo ya mashindano yenye heshima kubwa katika kanda ya Afrika Kaskazini.
Habari ID: 3481414    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/25

IQNA – Kwa kuboresha mazingira ya upangaji na uamuzi, na kuongeza ushiriki wa washiriki wenye hamasa, mashindano ya kuhifadhi Qur’ani ya Australia yamegeuka kuwa mfano bora wa kuimarisha utambulisho wa vijana Waislamu nchini humo.
Habari ID: 3481410    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/24

IQNA – Waziri wa Mambo ya Waqf wa Misri ametoa pongezi zake kwa kuenziwa hivi karibuni kwa Qari maarufu Sheikh Abdul Fattah Taruti wakati wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yaliyofanyika mjini Moscow, Russia
Habari ID: 3481409    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/24

IQNA – Katika tukio la kihistoria lililopeperushwa kupitia kipindi cha televisheni cha Ahl Masr nchini Misri, tafsiri ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa mkono na mwanazuoni mashuhuri wa Al-Azhar, marehemu Sheikh Ahmed Omar Hashem, imewasilishwa kwa mara ya kwanza hadharani. Kazi hiyo ya miaka kumi imekamilika kabla ya kifo chake mapema mwezi huu.
Habari ID: 3481404    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/23

Ushirikiano katika Qur’ani Tukufu/4
IQNA – Ushirikiano na usalama wa kijamii kwa wale waliotengwa na wahitaji ni miongoni mwa masharti muhimu ya mwenendo wa waumini, kwa mujibu wa aya za Qur’ani Tukufu na Hadithi za Ahlul-Bayt (AS).
Habari ID: 3481395    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/21

IQNA – Kongamano la kwanza la kimataifa la “Qur’an ya Negel” limefanyika mjini Sanandaj siku ya Jumatatu, likiwakutanisha makari na wahifadhi wa Qur’an wanaozungumza Kikurdi kutoka Iran, Uturuki na Iraq.
Habari ID: 3481394    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/21

IQNA – Bi Zubaydah Taysert, Waziri wa Utamaduni wa Thailand, alifanya ziara rasmi katika Makumbusho ya Urithi wa Kiislamu na Kituo cha Elimu ya Qur'ani kilichoko katika wilaya ya Yingluck, Jumamosi tarehe 18 Oktoba 2025, kabla ya uzinduzi rasmi wa majengo hayo.
Habari ID: 3481389    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/20

IQNA – Usajili umefunguliwa kwa toleo la 30 la Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikh Jassim bin Muhammad bin Thani nchini Qatar.
Habari ID: 3481388    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/20

IQNA-Katika mji wa Mason, jimbo la Ohio nchini Marekani, kuna shule inayojulikana kama ICM Learning Academy ambayo hufundisha wanafunzi si tu kusoma Qur’ani Tukufu bali pia kuifahamu na kuikumbuka kwa moyo wote.
Habari ID: 3481384    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/19

Ushirikiano katika Qur’ani Tukufu/3
IQNA-Katika Aya ya pili ya Surah Al-Ma’idah, Mwenyezi Mungu Mtukufu ametaja amri nane muhimu, ambazo ni miongoni mwa maagizo ya mwisho aliyoteremshiwa Mtume Muhammad (Rehema na Amani zimshukie). Miongoni mwa amri hizo ni kushikamana kwa pamoja katika njia ya wema na uchamungu.
Habari ID: 3481383    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/19

IQNA-Wizara ya Wakfu wa Kidini ya Misri imemteua rasmi Qari Dkt. Ahmed Ahmed Nuaina kuwa Sheikh al-Qurra, yaani Kiongozi Mkuu wa Wasomaji wa Qur'anI nchini humo.
Habari ID: 3481377    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/17

IQNA – Tarehe 15 Oktoba, katika Msikiti Mkuu wa Astana, Kazakhstan, mashindano ya pili ya Kimataifa ya Usomaji na Kuhifadhi Qur'an Tukufu yamekamilika, yakileta pamoja washiriki 22 kutoka mataifa 21. Tukio hili limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Kiislamu ya Saudi Arabia na Mamlaka ya Kiroho ya Waislamu wa Kazakhstan.
Habari ID: 3481374    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/17