qurani tukufu - Ukurasa 8

IQNA

IQNA – Ifuatayo ni qiraa ya tartili ya Juzuu ya Sita ya Qur’ani Tukufu, ambayo imesomwa na qari mashuhuri wa Iran, Ustadh Qassem Moqaddami. Jiungeni na IQNA kila siku katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa safari ya kiroho kupitia Qur’ani Tukufu, kwa lengo la kukamilisha au kuhitimisha usomaji wa Qur’ani nzima ifikapo mwisho wa mwezi huu uliobarikiwa.
Habari ID: 3481987   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/24

IQNA – Katika tukio nadra linaloonesha upanuzi unaokua wa elimu ya Qur’ani katika ngazi ya kimataifa, mji mkuu wa Rwanda uliandaa hafla ya kuhitimu wahifadhi wa Qur’ani 70,000, wanaume na wanawake.
Habari ID: 3481968   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/21

IQNA – Mpango mkubwa nchini Malaysia wa kusambaza nakala milioni moja za Qur'ani Tukufu kupitia mfumo wa waqf unakaribia kufikia lengo lake la mwisho kwa kasi kubwa.
Habari ID: 3481964   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/20

IQNA – Ataba (uongozi na usimamizi) wa Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS) mjini Karbala, Iraq, umetangaza kukamilika kwa maandalizi yote ya kuandaa hafla ya Khatm Qurani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3481963   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/20

IQNA – Wakati ustadi wake wa kuchezesha mpira unawatia mshangao mabeki uwanjani, Amad Diallowinga wa timu ya Ligi Kuu ya Uingereza, EPL, Manchester United anabainisha kuwa chanzo chake cha kweli cha nguvu na uthabiti kinatokana na imani yake.
Habari ID: 3481962   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/20

IQNA – Ifuatayo ni qiraa ya tartili ya Juzuu ya Pili ya Qur’ani Tukufu, ambayo imesomwa na qari mashuhuri wa Iran, Ustadh Qassem Moqaddami. Jiungeni na IQNA kila siku katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa safari ya kiroho kupitia Qur’ani Tukufu, kwa lengo la kukamilisha au kuhitimisha usomaji wa Qur’ani nzima ifikapo mwisho wa mwezi huu uliobarikiwa.
Habari ID: 3481960   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/20

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amehudhuria kikao cha kiroho cha Qur'ani katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, akijumuika na maqarii na wasomaji mashuhuri wa Iran na kimataifa wa Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3481959   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/20

IQNA — Video iliyosambaa siku ya Jumanne inaonyesha mlowezi Mzayuni akichoma nakala ya Qur’ani Tukufu katika mji wa al‑Quds (Jerusalem), kitendo cha makusudi cha kudharau kitabu kitakatifu cha Waislamu ambacho kinahatarisha kuchochea mvutano mkubwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3481955   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/18

IQNA — Wizara ya Awqaf ya Misri imetangaza kuwatuma wasomaji wa Qur’ani na maimamu katika nchi 22 wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3481953   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/18

IQNA –Sambamba na kuonekana kwa mwezi mwandamo unaoashiria kuingia kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, watazamaji nchini Qatar na nje ya nchi hiyo watapata mwandani mpya wa kiroho.
Habari ID: 3481949   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/17

IQNA – Mkuu wa Maonyesho ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran amesema kuwa kuendeleza mtindo wa maisha wa Kiirani-Kiislamu na kuimarisha diplomasia ya Qurani ni miongoni mwa malengo makuu ya toleo hili.
Habari ID: 3481948   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/17

IQNA – Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) limesambaza kionjo rasmi cha msimu mpya wa kipindi cha televisheni cha “Mahfel”, ambacho hurushwa nchini Iran wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3481943   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/16

IQNA – Hafla maalumu ilifanyika nchini Yemen kuwaenzi wanafunzi 200 waliokamilisha masomo yao katika vikao vya Qur’ani vilivyoendeshwa misikitini katika kitongoji cha Madhbah, Wilaya ya Maeen.
Habari ID: 3481939   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/15

IQNA – Mutawalli wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) amesisitiza kuwa kulea na kukuza haiba au shakhsia ya Kiislamu kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu ni msingi wa kujenga jamii kamilifu na yenye fadhila.
Habari ID: 3481935   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/14

IQNA – Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamegeuka kuwa mfano hai wa kuunganisha dini, maisha ya kijamii na maendeleo katika ulimwengu wa kisasa, amesema mchambuzi mmoja wa masuala ya kisiasa kutoka Lebanon.
Habari ID: 3481925   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/12

IQNA – Kituo cha Sheikha Hessa Bint Ali Al Khalifa cha Kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Kufundisha Sayansi za Qur’ani kimefunguliwa rasmi kwa ajili ya wanawake katika eneo la Al‑Bustain, mkoa wa Muharraq, nchini Bahrain.
Habari ID: 3481924   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/12

IQNA – Shambulio la ndege zisizo na rubani au droni lililolenga msikiti na kituo cha kuhifadhi Qur’ani katika jimbo la Kordofan Kaskazini nchini Sudan limesababisha vifo vya watoto watatu na kujeruhi wengine 13.
Habari ID: 3481921   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/12

IQNA – Ingawa kipindi cha vipaji vya Qur’ani cha Misri “Dawlat El‑Tilawah" bado hakijafikia hatua ya fainali, Maqari au wasomaji wawili waliobainika kwa umahiri wao katika kipindi hicho walitunukiwa zawadi katika hafla rasmi iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Cairo.
Habari ID: 3481917   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/11

IQNA – Mashindano maalum ya Qur'ani yaliyobuniwa mahsusi kwa watu wenye usonji wa Down yamefanyika kwa mafanikio makubwa mjini Benghazi, Libya, yakilenga usomaji wa Qurani, hifadhi ya Qurani, na Adhana.
Habari ID: 3481915   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/10

IQNA – Jumuiya ya Qur'ani ya Iran imesisitiza kuwa vita kuu duniani hadi leo bado ni vita juu ya Qur'ani, ikisema kuwa hali ya sasa ya maendeleo ya kimataifa inaonyesha wazi kuwa wakati umefika kwa mazungumzo na fikra za Qur'ani kujitokeza kwa nguvu katika uwanja wa umma.
Habari ID: 3481913   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/10