qurani tukufu - Ukurasa 2

IQNA

IQNA – Ali Qassem ni mwandishi wa hati (khatati au kaligrafia) kutoka nchini Yemen ambaye amejitolea katika kuhifadhi mapokeo ya kale ya uandishi wa Qur’ani Tukufu kwa kutumia hati ya Kiuthmaniya (Rasm al-Uthmani).
Habari ID: 3482548   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/28

IQNA - Kozi ya Qur’ani imefanyika mjini Karbala, Iraq, kwa lengo la kuimarisha ujuzi wa majaji wanawake wa mashindano ya Qur’ani.
Habari ID: 3482547   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/28

IQNA – Sheikh Awad Abdullah Al-Faradi si mshiriki mwenye umri mkubwa zaidi pekee, bali pia ndiye aliyewavutia na kuwapa hamasa kubwa zaidi wengi katika Mashindano ya televisheni ya Qur’ani Tukufu ya Misri ambayo ni maarufu kama Dawlat al-Tilawa.
Habari ID: 3482541   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/26

IQNA – Mbunge mmoja wa Malaysia kutoka jimbo la Sarawak amesisitiza umuhimu wa kizazi kipya kujifunza kusoma na kuelewa Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3482533   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/25

IQNA – Hafla maalumu imeandaliwa kwa ajili ya kuwatunuku zawadi na kuwaenzi vijana 600 waliohifadhi Qur’ani Tukufu katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3482530   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/24

IQNA – Tarjuma na tafsiri za Qur’ani Tukufu katika lugha 44 zimewekwa mtandaoni na zinapatikana bure bila malipo.
Habari ID: 3482528   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/24

IQNA– Katika mwendelezo wa kuenzi utamaduni wa kuhifadhi Qur'ani Tukufu, matembezi makubwa ya wahifadhi wa Qur'ani yamefanyika katika mji wa Tifelt, Morocco, ili kusherehekea wahitimu waliofanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu. Tukio hilo la kiroho liliambatana na mahudhurio ya viongozi wa kidini, maafisa wa serikali, na wakazi wa mji huo, kama ilivyoripotiwa na Tifeltpress.
Habari ID: 3482525   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/22

IQNA – Katika mwendelezo wa kuimarisha utamaduni wa elimu ya Kiislamu, sherehe ya kipekee imefanyika katika mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott, kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi 45 kutoka eneo la Amboud (M’Bout) ambao wamefanikiwa kuhifadhi Qur'an Tukufu kikamilifu.
Habari ID: 3482522   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/22

IQNA – Mashindano ya 18 ya kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu nchini Bosnia na Herzegovina yalihitimishwa katika hafla iliyofanyika katika mji mkuu, Sarajevo.
Habari ID: 3482517   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/21

IQNA – Mtaalamu na msomaji maarufu wa Qur’ani wa Iran amemuelezea Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kama kielelezo cha maisha ya Qur’ani katika zama zetu za kisasa.
Habari ID: 3482513   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/20

IQNA – Katika Khitma ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, iliyofanyika katika Haramu Tukufu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, Qari mashuhuri wa Iran, Ustadh Ahmad Abolqassemi, aliongoza usomaji wa aya za 64 hadi 71 za Surah An-Nisa pamoja na Surah Al-Fatiha.
Habari ID: 3482511   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/19

IQNA – Gavana wa Dakahlia, nchini Misri, amemtunuku nakala ya Qur’ani Tukufu Imam Ashour, mchezaji wa timu ya taifa ya Misri na klabu ya Al-Ahly, ikiwa ni ishara ya kutambua juhudi zake katika Kombe la Dunia la mwaka 2026.
Habari ID: 3482508   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/19

IQNA – Msururu wa usomaji wa Qur’ani wenye kuvutia ambao uliwapagawisha majaji na hadhira kwa pamoja umeshuhudiwa katika raundi za awali za msimu wa pili wa shindano la “Dawlet El-Tilawa” (Dola ya Usomaji) nchini Misri. Tukio hili linadhihirisha kipaji cha kipekee na juhudi za hali ya juu za washiriki kutoka sehemu mbalimbali za nchi hiyo katika kulihudumia Kitabu Kitukufu.
Habari ID: 3482503   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/18

IQNA – Katika kuamsha ari ya mapenzi ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu wakati wa likizo ya kiangazi, Chuo cha Tahfidh cha “Little Memorizers” (Wahifadhi Wadogo) mjini Pristina, kinachofanya kazi chini ya usimamizi na usimamizi wa kiroho wa Msikiti Mkuu wa Kosovo, kimezindua rasmi programu yake maalum ya “Darsa za Kiangazi za Mwaka 2026.”
Habari ID: 3482492   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/15

IQNA – Shule mpya ya Qur’an imezinduliwa katika eneo la Myrza-Ake, katika mji wa Uzgen, Mkoa wa Osh, nchini Jamhuri ya Kyrgyzstan.
Habari ID: 3482490   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/15

IQNA – Chuo Kikuu cha Qur’ani na Shule ya Mafunzo ya Kidini cha Juu kimefunguliwa katika mji wa Rida, mkoani Bayda, nchini Yemen, Jumapili.
Habari ID: 3482487   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/14

IQNA – Makumbusho mapya katika Eneo la Kitamaduni la Hira jijini Makka yanawazamisha wageni katika bahari ya historia ya uandishi wa Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3482486   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/14

IQNA – Maktaba ya Alexandria imeandaa kongamano lililopewa anuani ya: “Usomaji wa Qur’ani nchini Misri; Utafiti wa Ukuzaji na Kuporomoka Kwake,” ikiwa ni sehemu ya programu ya kiutamaduni katika Maonesho ya Vitabu ya Kimataifa ya maktaba hiyo.
Habari ID: 3482485   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/14

IQNA – Kundi la waumini wanaotekeleza Hija ndogo ya Umrah lilitembelea siku ya Jumamosi Kituo cha Mfalme Fahd cha Uchapishaji wa Qur’ani Tukufu mjini Madina.
Habari ID: 3482477   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/13

IQNA – Kituo cha Qur’ani cha Al-Nour kilichopo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kinaendelea na shughuli zake za kutoa elimu ya Kiislamu licha ya changamoto chungu nzima zinazotokana na vita vya kikatili.
Habari ID: 3482476   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/12