IQNA – Maqari wa kike wa Qur’ani kutoka Dar-ul-Qur’an ya Astan ya Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) wameibuka washindi katika mashindano ya saba ya kitaifa ya wanawake wa Qur’ani nchini Iraq.
Habari ID: 3481531 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/17
IQNA-Duru ya tatu kwa mashindano ya kila mwaka ya Qur’ani nchini Nepal imeingia hatua ya mwisho, Jumapili. Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Da‘wa na Mwongozo ya Saudi Arabia imezindua raundi ya mwisho ya mashindano ya kuhifadhi Qur’ani kwa wavulana na wasichana katika mji mkuu wa Katmandu, ulioko Asia Kusini.
Habari ID: 3481530 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/17
IQNA – Kipindi cha televisheni Dawlet El Telawa, mashindano maalum ya vipaji vya usomaji wa Qur’ani nchini Misri, kimemkumbuka Qari maarufu Sheikh Mahmud Khalil al‑Hussary.
Habari ID: 3481526 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/16
IQNA – Je, ni vipi maandishi ya kidini kama Qur’ani Tukufu yanaweza kuthibitishwa kuwa sahihi na kusomwa kwa kutumia akili mnemba (AI) ya kisasa?
Habari ID: 3481525 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/16
IQNA-Vehbi Ismail Haki (1919–2008) alikuwa mwandishi, imam na msomi mashuhuri kutoka Albania aliyechangia pakubwa kusambaza utamaduni wa Kiislamu na maarifa ya Qur’ani kwa watu wa taifa lake kupitia maandiko kwa Kiarabu, Kiingereza na Kialbania. Alizaliwa Shkodra, mji wa kaskazini wenye historia ndefu ya elimu ya Kiislamu tangu enzi za Waothmani.
Habari ID: 3481523 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/16
Ushirikiano katika Qur’ani Tukufu / 11
IQNA – Ushirikiano na watu binafsi pamoja na taasisi zinazojitahidi kuandaa mazingira ya ndoa na kuundwa kwa familia kwa vijana ni miongoni mwa mifano dhahiri ya ushirikiano wa kijamii.
Habari ID: 3481521 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/15
IQNA – Katika ujumbe wake kwa washiriki wa mashindano ya 17 ya kitaifa ya Qur’ani “Mudha Mattan”, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt. Masoud Pezeshkian, ameyataja mashindano hayo kuwa ni uwanja wa kukuza ushirikiano, huruma, na kuendeleza stadi mbalimbali za kufanya kazi kwa pamoja.
Habari ID: 3481519 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/15
Qur’ani ni Chemchemi ya Maarifa
IQNA – Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Iran amesisitiza kuwa akili mnemba (AI) inapaswa kutumika kwa lengo la kuendeleza Qur’ani Tukufu, akibainisha kuwa jukumu hilo ni huduma muhimu ya kielimu kwa Uislamu.
Habari ID: 3481517 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/15
IQNA – Wavamizi wa Kizayuni wasiokuwa halali waliharibu msikiti katika mji wa Deir Istiya, Ukingo wa Magharibi, usiku wa Alhamisi, wakichoma sehemu za ndani na kuharibu nakala kadhaa za Qur’ani Tukufu katika shambulio la dharau lililoambatana na maandiko ya vitisho.
Habari ID: 3481516 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/14
IQNA – Qur’an Tukufu ni ramani ya kuishi maisha mema, amesema mwanazuoni wa Kiislamu nchini Iran, akiongeza kuwa wale wanaoshikamana zaidi na Qur’ani huishi maisha ya heri na ya uadilifu yanayopendeza kwa Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3481515 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/14
IQNA – Wizara ya Awqaf na Mambo ya Kiislamu ya Qatar imezindua maonyesho ya Qur’an sambamba na toleo la 30 la Mashindano ya Qur’an ya Sheikh Jassim bin Mohammed Al Thani mjini Doha.
Habari ID: 3481514 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/14
IQNA – Qari mashuhuri wa Misri, Abdul Fattah Tarouti, amemuelezea marehemu Sheikh Abdul Fattah Sha’sha’i kuwa ni msomaji wa Qur’an aliyebeba sauti ya kipekee na ya kifahari, iliyodhihirisha ukubwa wa Qur’an na kuasisi mtindo wa kipekee wa qira’a.
Habari ID: 3481512 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/14
IQNA – Kipindi cha televisheni kiitwacho “Dawlat al Telawah”, ambacho ndicho shindano kubwa zaidi cha vipaji vya usomaji na tartiil ya Qur’ani, kimepangwa kurushwa kupitia vituo vya satelaiti vya Misri.
Habari ID: 3481511 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/13
Ushirikiano Katika Qur’ani Tukufu/10
IQNA – Mifano ya ushirikiano unaojengwa juu ya msingi wa kheri na uchamungu, kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, haijabana tu katika kutoa mali na sadaka kwa masikini na wahitaji. Bali, kama kanuni ya jumla, ushirikiano huu una upeo mpana unaogusa masuala ya kijamii, kisheria, na kimaadili.
Habari ID: 3481503 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/11
IQNA – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amejibu ripoti ya gazeti la New York Times kuhusu kufukuzwa kwa baadhi ya majenerali wa Marekani kwa kunukuu aya ya Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3481502 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/11
IQNA – Mpango mpya wa kielimu uitwao Furqan umeanzishwa mjini Nouakchott kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi yatima kuboresha uwezo wao wa kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3481501 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/11
IQNA – Msikiti Mkuu wa Al-Azhar umetangaza uzinduzi wa matawi mapya 70 ya Taasisi ya Kuhifadhi Qur’ani ya Al-Azhar katika miji mbalimbali ya Misri.
Habari ID: 3481499 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/11
IQNA – Mradi wa kutafsiri Qur'an kwa lugha ya Rohingya umeanzishwa katika mazingira ambapo Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakilengwa na dhulma na kufukuzwa kutoka ardhi yao kwa miongo kadhaa. Lengo lake ni kuziba pengo la maarifa ya Kiislamu na kupambana na ukandamizaji wa lugha ya Rohingya.
Habari ID: 3481493 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/09
IQNA – Kituo cha Uchapishaji na Usambazaji wa Qur'an Tukufu cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimeanza kutumia teknolojia za Akili Mnemba (AI) kwa ajili ya kutengeneza nakala za Qur'ani za kidijitali, hatua inayofungua ukurasa mpya wa kuunganisha urithi wa kiroho na ubunifu wa kisasa.
Habari ID: 3481490 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/09
Ushirikiano Katika Qur’ani Tukufu /9
IQNA – Qur’ani Tukufu inakataza waziwazi aina yoyote ya ushirikiano katika maovu au uonevu. Katika Surah Al-Ma’idah aya ya 2, Allah anasema: “Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”
Habari ID: 3481488 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/08