qurani tukufu - Ukurasa 10

IQNA

IQNA – Toleo la pili la mkutano wa kimataifa kuhusu “Tafsiri ya Qur’ani na Akili Mnemba” linatarajiwa kufanyika nchini Morocco.
Habari ID: 3481845   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/25

IQNA – Nakala ya kihistoria na yenye thamani kubwa ya Qur'ani Tukufu, inayojulikana kama “Qur'ani ya Kufi,” imewekwa wazi kwa umma katika Makumbusho ya Qurani ya Makka.
Habari ID: 3481840   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/24

IQNA – Aplikesheni mahiri ya “Al Moeen” imezinduliwa katika hafla maalumu iliyofanyika Alhamisi katika Chuo cha Qur’ani Tukufu mjini Sharjah, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Habari ID: 3481837   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/23

IQNA-Hafla ya kuanza kurekodi qiraa au usomaji wa Qur’ani Tukufu kwa mtindo wa tartīl kwa riwaya za Warsh na Qālūn imefanyika katika Redio ya Mauritania.
Habari ID: 3481831   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/21

IQNA – Kikao cha usomaji wa Qurani kimefanyika katika Msikiti wa Hazrat Abulfadh (AS) mjini Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran, tarehe 19 Januari 2026, kwa mnasaba wa Eid al-Mab’ath, siku ya kukumbuka kutumwa kwa Muhammad (SAW) kuwa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3481826   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/20

IQNA – Maonyesho yenye kichwa “Shahidi wa Qur’ani” yameandaliwa katika mkoa wa al-Hudaydah, Yemen, yakitoa heshima kwa Sayyid Hussein Badreddin al-Houthi, ambaye nchini humo anajulikana kama shahidi wa Qur’ani.
Habari ID: 3481815   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/18

IQNA – Kitivo cha Lugha cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri kinaendeleza mradi mahsusi wa tafsiri na tarjuma unaolenga kuufikisha ujumbe wa Qur’ani Tukufu kwa mataifa mbalimbali duniani.
Habari ID: 3481798   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13

IQNA – Jumuiya ya Qur’ani ya Iran imelaani vikali machafuko mabaya yaliyotokea hivi karibuni nchini. Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, jumuiya hiyo iliwashukuru vikosi vya ulinzi na usalama kwa juhudi zao za kurejesha utulivu na amani katika jamii.
Habari ID: 3481793   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/12

IQNA-Kongamano la pili la Siku ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu limefanyika Jumapili 11 Februari jijini Qum, Iran, sambamba na kukaribia tarehe 27 Rajab ambayo inatambuliwa kama Siku ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ukumbi wa Bibi Fatima al‑Ma‘suma (SA.)
Habari ID: 3481791   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/12

IQNA – Kifaa kipya cha kielektroniki cha eBraille kilichotengenezwa nchini Malaysia kimeleta mageuzi makubwa katika kujifunza Qur'ani Tukufu kwa watu wenye uoni hafifu, au ulemavu wa macho kwa kuwapa uwezo wa kupata maandiko ya dini moja kwa moja kwa njia ambayo haijawahi kupatikana hapo awali, sambamba na kufungua fursa katika nyanja nyingine za elimu.
Habari ID: 3481789   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/11

IQNA – Msimamizi mkuu wa mashindano ya vipaji vya Qur’ani nchini Misri, maarufu kwa jina “Dawlat al-Tilawa”, ametangaza kuwa msimu mpya wa kipindi hicho kitaanza rasmi Novemba 2026.
Habari ID: 3481784   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/08

IQNA – Mwana wa qari maarufu wa Misri aliyefariki, Abdul Basit Abdul Samad, amepongeza kuanzishwa kwa Jumba la Makumbusho la Waqari wa Qur’an nchini humo.
Habari ID: 3481782   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/08

IQNA – Kiwanda cha Mfalme Fahd cha Kuchapisha Qur’an kilichoko mjini Madina, Saudi Arabia, kilipokea wageni wapatao milioni moja kutoka ndani na nje ya nchi mwaka uliopita.
Habari ID: 3481779   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/07

IQNA – Ili kuunga mkono ndoa na familia, mjasiriamali mmoja kutoka Jordan ametangaza kuwa vijana watakaohifadhi juzuu sita za Qur’ani Tukufu watapewa msaada wa kifedha pindi watakapooana.
Habari ID: 3481775   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/06

IQNA – Televisheni ya Thaqalayn Satellite imetangaza mpango wa kuandaa mashindano ya tatu ya kimataifa ya Qur’ani yanayojulikana kama “Wa Rattil” katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.
Habari ID: 3481774   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/06

IQNA – Kipindi cha 12 cha mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Dawlat al-Tilawa nchini Misri kiligeuka safari ya kiroho na kihisia, ambapo simulizi binafsi ziliungana na sauti za mbinguni, zikazalisha athari ya kina iliyogusa nyoyo za kila msikilizaji.
Habari ID: 3481773   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/06

IQNA – Mjadala maalum kuhusu “Wajibu wa Umma wa Kiislamu katika kukabiliana na udhalilishaji wa Qur’ani na matukufu mengine na maadui” umefanyika mjini Sanaa, mji mkuu wa Yemen.
Habari ID: 3481772   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/06

IQNA – Toleo la 26 la Mashindano ya Kuhifadhi Qur’ani nchini Japan limefanyika chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Waislamu wa Japan.
Habari ID: 3481771   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/05

IQNA – Mashindano ya Qur’ani kwa wanafunzi wa kiume na wa kike kutoka shule za serikali na binafsi yameanza Jumapili katika Mkoa wa Hodeidah, Yemen.
Habari ID: 3481770   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/05

IQNA – Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina, qari mashuhuri wa Misri, amechapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook video inayoonyesha mwanamke Mmarekani akisilimu katika moja ya misikiti nchini Marekani.
Habari ID: 3481769   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/05