qurani tukufu - Ukurasa 9

IQNA

IQNA – Omar Ali Awad ametangazwa na kutunukiwa tuzo ya “Tawi la Dhahabu” katika shindano la vipaji vya Qur’ani lijulikanalo kama “Dawlet El Telawa (Hali ya Usomaji)” nchini Misri.
Habari ID: 3481903   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/08

IQNA – Meya wa Jiji la New York, Zahran Mamdani, ametetea agizo lake linaloweka mipaka kwa ukamataji unaofanywa na maafisa wa Idara ya Uhamiaji na Forodha ya Marekani (ICE), akieleza kuwa ulinzi wa wahamiaji si suala la kisera pekee, bali ni wajibu wa kimaadili unaochochewa na mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Hijra ya Mtume Muhammad (rehema na amani ziwe juu yake) kwenda Madina.
Habari ID: 3481900   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/08

IQNA-Malaysia inaendelea kutumia diplomasia ya kitamaduni na kidini kwa kusambaza nakala 40,000 za Qur’ani Tukufu zenye tarjuma katika lugha mbali mbali huko Marekani na Afrika Magharibi.
Habari ID: 3481898   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/07

IQNA-Malaysia iko mbioni kuanzisha chuo kikuu maalumu kwa elimu za Qur’ani, kufuatia ridhaa ya Sultan wa Pahang ya kubadilisha jina la taasisi ya elimu iliyopo tayari.
Habari ID: 3481897   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/07

IQNA – Wageni wa Jumba la Makumbusho ya Qur’ani Tukufu katika Wilaya ya Kitamaduni ya Ḥirā’, mjini Makka, sasa wanayo fursa ya kushuhudia turathi adhimu iliyovunja rekodi ya dunia: nakala ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa kwa mkono, iliyo kubwa zaidi kuliko zote duniani, ambayo sasa inaonyeshwa rasmi kwa umma.
Habari ID: 3481893   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/05

Mwokozi katika Qur’ani Tukufu / 1
IQNA – Aya ya 55 ya Surat An-Nur inaeleza juu ya jamii tukufu ambayo bado haijawahi kutimia kikamilifu katika ulimwengu huu, wala haiwezi kutekelezwa juu ya jamii yoyote ile isipokuwa ile itakayoundwa kwa baraka ya kudhihiri kwa Imamu Mahdi (AS).
Habari ID: 3481892   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/05

IQNA — Toleo la tisa la Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani na Ibtihal ya Port Said limehitimishwa, ambapo washiriki kutoka Misri wameibuka kidedea kwa kushinda nafasi ya kwanza katika makundi yote matatu ya mashindano hayo.
Habari ID: 3481884   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/03

IQNA – Mfungwa mmoja katika mkoa wa Balıkesir, nchini Uturuki, amefikia daraja ya Hafidh, baada ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu yote kupitia mpango wa elimu ya magerezani unaoungwa mkono na serikali.
Habari ID: 3481870   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/30

IQNA – Yatima arobaini na wanane nchini Jordan wamepata thawabu tukufu ya safari ya Umrah iliyogharamiwa kikamilifu, baada ya kung’ara katika mashindano ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3481869   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/30

IQNA – Hafla maalumu ilifanyika katika Msikiti wa Barduşit mjini Pristina, mji mkuu wa Kosovo, kwa lengo la kuwaenzi wanafunzi 80 wa kike wa Qur’ani walioshiriki katika duru za masomo ya Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3481866   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/29

IQNA – Chuo Kikuu cha Jamia Millia Islamia (JMI) mjini New Delhi, India, kilizindua rasmi kongamano kubwa la kimataifa la siku tatu siku ya Jumatano, likiwakusanya wasomi na wanazuoni kutoka pembe mbalimbali za dunia ili kuchambua kwa kina uhusiano hai kati ya mafundisho ya Qur’ani Tukufu na maendeleo ya sayansi ya kisasa.
Habari ID: 3481865   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/29

IQNA – Mlipuko mkubwa wa fataki uliomkumba Eiman Najwan Anwar Fuad ulimnyang’anya uwezo wa kuona na kuharibu mikono yake akiwa na umri wa miaka 22.
Habari ID: 3481863   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/29

IQNA – Nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa mfumo wa nukta nundu (Braille) zinasambazwa kwa wageni wanaotembelea Maonesho ya 57 ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo mwaka 2026.
Habari ID: 3481862   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/29

IQNA – Mamlaka ya Fatwa ya Misri (Dar al‑Ifta) imetangaza kwamba matumizi ya programu za akili mnemba (AI), ikiwemo ChatGPT, katika kufasiri Qur’ani Tukufu hayaruhusiwi kisheria.
Habari ID: 3481861   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/28

IQNA – Akilaani matukio ya hivi karibuni ya kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu, mwanaharakati wa Qur’ani kutoka Iran ametoa wito wa kuundwa kwa Jumuiya ya Kimataifa wa Maqari wa Qur’ani ambayo miongoni mwa majukumu yake ni kufuatilia hatua za kisheria dhidi ya vitendo hivyo.
Habari ID: 3481856   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/27

IQNA-Mashindano ya Qur’ani kwa wasichana yamefanyika katika mkoa wa Hajjah nchini Yemen, yakionyesha juhudi za kuimarisha elimu ya Qur’ani miongoni mwa wanafunzi wa kike.
Habari ID: 3481855   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/27

IQNA – Waziri wa Mambo ya Dini na Awqaf wa Algeria amewakabidhi wanazuoni wa Afrika nakala ya kihistoria ya Qur'ani Tukufu ijulikanayo kama “Rhodosi”, wakati wa kongamano lililofanyika nchini humo kuhusu diplomasia ya kidini.
Habari ID: 3481851   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/26

IQNA – Nakala 114 adimu za Qur'ani Tukufu kutoka nchi 44 zimewekwa katika maonyesho maalumu yanayofanyika mjini Istanbul, Uturuki.
Habari ID: 3481850   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/26

IQNA – Jumuiya ya Watumishi wa Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani machafuko ya hivi karibuni yaliyoungwa mkono na tawala zakigeni, na ikalisifu taifa la Iran kwa kuvuruga njama za maadui.
Habari ID: 3481849   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/26

IQNA – Ensaiklopidia Maalumu ya Usomaji wa Qur’ani na Sayansi Zake imezinduliwa na Qatar kama kazi mpya inayolinda uhalisia wa kielimu huku ikileta urithi wa qira’ah katika muundo wa kidijitali kwa watafiti na wapenda taaluma za Qur’ani.
Habari ID: 3481848   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/26